Header Ads Widget

RADI YAUA 3 NA KUJERUHI 19 WAKIWA KWENYE MATANGA - LINDI

  

Watu watatu wamefariki Dunia papo hapo na wengine 19 kujeruhiwa kwa kupigwa na kuunguzwa na  Radi wakiwa kwenye Matanga ya msiba katika kijiji cha Nahukahuka Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi .

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi kwa waandishi wa habari inasema tukio hilo limetokea jana February 9 majira ya saa tisa jioni huko katika kijiji cha Nahukahuka ambapo watu hao walikuwa kwenye Matanga ya msiba nyumbani kwa Idrisa Lubuva.


Waliofaliki katika Ajali hiyo ni Rukia Hassan (59)Abdallah Liputa(18) Mustafa Mwalimu (2) wote ni wakazi wa Nahukahuka.

Kwa upande wake Dokta Abdallah Mputa Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Nyangamara amekiri kupokea miili ya Marehemu 3 na majeruhi 19 waliofikishwa hospitalini hapo siku ya tarehe 9/02/2024 majira ya saa 10 jioni .

Amesema kati ya majeruhi 19 waliopokelewa kituoni hapo 13 kati yao wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea Nyumbani kwao na watu 6 wanaendelea kupatiwa matibabu.


Kuhusu marehe amesema Baada ya miili yao kufanyiwa uchunguzi imebainika sababu ya kifo chao ni kupigwa na kuunguzwa na radi na kupelekea Damu na maji kukauka mwilini

Hata hivyo Dkt. Mputa alisema kuwa miili ya marehemu imeshakabidhiwa kwa ndugu tayari kwa taratibu za mazishi



Mwisho 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI