Nyumba inayodaiwa kuwa ya mkurugenzi wa gazeti la Tanzania daima, Dudley Mbowe iliyopo Mikocheni, jijini Dar es salaam, imekamatwa kwaajili ya kupigwa mnada, ili kulipa deni la malimbikizo ya mishahara ya waliokuwa waandishi na wahariri wa gazeti hilo, shilingi milioni 62.7
Nyumba hiyo ya ghorofa moja iliyopo katika kiwanja namba 9, mtaa wa feza, Barabara ya Chipata, mikocheni A imekamatwa leo jumatano, February 28, 2024 na dalali wa mahakama, kampuni ya udalali ya MM Auctioneer & Debt Collectors.
Dalali alifika katika nyumba hiyo saa 3:40 na kuegesha gari lake nje ya geti la nyumba hiyo.
Baada ya muda mfupi Dudley, ambaye nim toto wa Mwenyekiti wa chadema Freeman Aikael Mbowe alitoka nje na kumfuata dalali huyo aliyejitambulisha na jukumu alilokwenda kulitekeleza eneo hilo.
0 Comments