Amesema Mafunzo hayo kuwepo ni mchakato wa muda Marefu nani muhimu kwa watoa huduma kwani kumekuwepo na malalamiko kwa abiria. "Tumeona kunauhitaji mkubwa wa kuhakikisha watoa huduma kwenye mabasi wanapatiwa Mafunzo ili wasafiri waweze kufurahia safari zao lakini pia kumaliza malalamiko yanayoendelea kwa sasa, " Amesema Afisa Mfawidhi Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Mkoa wa Dodoma -Ndg. Ezekiel Emanuel amesema Mafunzo hayo yataleta mapinduzi chanya kwenye sekta ya usafirishaji . Amesema Mamlaka ya usafiri na usafirishaji Tanzania Latra wamekuwa na jukumu la kutatua migogoro wakipokea malalamiko kutoka kwa wapokea huduma ambao ni abiria. " Watoa huduma kwenye mabasi ya Masafa Marefu wamekuwa wakitoa huduma iliyochini ya kiwango na hiyo yote ni kutokana na kutokuwa na elimu sahihi ya huduma kwa mteja ni ni ni, " Amesema na kuongeza " Niwaombe wamiliki wa magari ya usafirishaji wajitahidi kuwapeleka watoa huduma kupata Mafunzo ya huduma kwa wateja kwani kwakufanya hivyo itawasaidia kwenye biashara zao, " Amesema Naye Akizungumza mwakilishi wa Mkuu wa Chuo hicho ambaye ni Mkuu wa kituo cha Mafunzo ya Lojistiki na Biashara Dkt Prosper Nyaki amesema kozi hii ya muda mfupi itawajengea washiriki uwezo na umahiri katika kuzitambua sheria za LATRA na Kanuni zake, na utoaji wa
huduma bora kwa mteja, mbinu za utoaji wa huduma ya kwanza, usalama wa abiria na mali zao, utunzaji wa mizigo na utambuzi wa bidhaa hatarishi kwa kuzingatia kanuni za usafirishaji, namna bora ya kushughulikia malalamiko ya mteja, usafi na utunzaji wa mazingira, mahusiano na mawasiliano, nidhamu na unadhifu wa mtoa huduma, pamoja na maarifa ya utoaji na umuhimu wa tiketi mtandao.Amesema Mafunzo hayo ni endelevu na yatakua yakiendeshwa katika Kampasi ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji iliyopo Mabibo jijini Dar es Salaam kwa muda wa wiki mbili na gharama nafuu kwa kila mshiriki (kalenda ya mafunzo hayo pamoja na gharama inapatikana katika tovuti ya Chuo ambayo ni www.nit.ac.tz). Aidha Chuo kipo katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za mashirikiano na VETA ambapo kupitia mashirikiano hayo Chuo kitasogeza huduma zaidi kwa wadau kupitia kampasi za Vyuo vya VETA ambavyo vipo katika kanda zote za Tanzania"Kama tulivyobainisha katika tangazo la udahili, washiriki wote hawa wapatao 70 katika kanda hii ya Kati wamefadhiliwa na mradi ujulikanao kama East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP) unaoendeshwa na Chuo, " Na kuongeza "Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unatekelezwa katika nchi tatu yaani Tanzania, Kenya na Ethiopia ili kuwezesha muingiliano wa kijamii katika nchi za ukanda wa Afrika, " Aidha amesema katika kufikia malengo ya Mradi, Chuo kina majukumu ya Kuandaa Mitaala inayokidhi matakwa ya soko la ajira, kuongeza ushirikiano na Taasisi nyingine za ndani na nje ya nchi kwa kuwa na mikataba ya ushirikiano , Kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ,Kuzifikia Taasisi zingine ambazo ziko nje ya mradi na kutoa mafunzo ,Kuwajengea uwezo watumishi katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya nchi. Hivyo basi, katika kutekeleza malengo hayo ya mradi wa EASTRIP hususani lengo Na. IV, Chuo kimeandaa mafunzo haya kufanyikakatika Kanda sita za Tanzania ambapo washiriki watakaopata udahili katika kanda hizo watalipiwa ada ya mafunzo kupitia fedha za Mradi. Kanda hizo ni, Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro,Tanga nNaye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesemakuwa ,kuwepo kwa mafunzo hayo ni matokeo ya juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia waliowezesha kuwepo kwa Mradi huu wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project(EASTRIP) unaofadhiliwa na Beya Dunia ambao ni mkopo wa Serikali.
Aidha , ameupongeza Uongozi wa Chuo, wanataaluma na wafanyakazi wote kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuhakikisha kuwa mafunzo haya yanafanyika katika Mkoa wetu wa Dodoma kwa kanda hii ya Kati mngeweza kuamua yakafanyika mikoa mingine ya kanda hii, kwetu sisi ni heshima kubwa.Amesema Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kimepewa jukumu kubwa la kuwaandaa wataalamu waliobobea katika nyanja tano za usafirishaji. "Lakini leo nitajikita kwenye usafiri wa barabarani ambapo mmekuwa mkituzalishia wataalamu mbalimbali wenye weledi mkubwa.Ombi langu kwa Chuo ni kuhakikisha kinatoa mafunzo haya mara kwa mara ili wataalamu hawa waendelee kutoa huduma zinazo kidhi vigezo kwa abiria wao, " Amesema Senyamule.Na kuongeza " Nina hakika, ikiwa kila mmoja atatekeleza majukumu yake na kuyafanyia kazi yote niliyoyataja pamoja na mengineyo natumaini kwamba malalamiko ya wateja wenu yatapungua kwani ni muhimu kuzingatia yale mtakayojifunza ndani ya siku tano (5) hapa. Amesema ili kuweza kufanikiwa ni lazima kila mmoja aweze kusoma kwa bidii na kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu.

0 Comments