Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa mwili wa mtu aliyepoteza maisha katika ajali ya maji iliyotekea huko Miami, Marekani ni Abraham Mgowano mwenye umri wa miaka 35 raia wa Tanzania.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa polisi walipokea simu, kutoka eneo la tukio juu ya kuonekana kwa mwili unaoelea katika mto Miami, ikiwa ni siku tatu toka Mgowano aripotiwe kuanguka kutoka kwenye boti ya kitalii, aliyokuwemo na wenzake.
Imeelezwa kuwa kabla ya kutokea tukio hilo, Mgowano alikuwa na watu wengine kumi na tatu kwenye boti hiyo na muda mfupi baada ya kuzama vikosi vya uokoaji vikiwemo vya polisi, vilianzisha msako lakini hawakufanikiwa.
Taarifa ya Polisi imesema kijana huyo alikwenda Miami kwaajili ya kutalii akitokea mji wa Berkeley uliopo kaskazini mwa jimbo la California ambapo akaunti zake za mitandao ya kijamii zimeonyesha alikuwa akifanya kazi kama injinia katika kampuni ya Google (Software engineer).
0 Comments