Header Ads Widget

MADIWANI KIGOMA WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI KWA TIJA

Madiwani wa manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwa kwenye kikao cha kupitisha makisio ya bajeti ya mapato na matumizi ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2024/2025Na Fadhili Abdallah,Kigoma Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kali amewataka madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa miradi katika maeneo yao ili kuwezesha miradi hiyo kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa maeneo yao. Kali  alisema hayo katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo kilichokuwa kikipitisha makisio ya bajeti ya mapato na matumizi ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa madiwani wanalo jukumu kubwa katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hasa mapato ya ndani lakini pia wanao wajibu mkubwa wa kusimamia matumizi kwenye utekelezaji wa miradi kwa wananchi. Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji,Mgeni Kakolwa akihitimisha kikao hicho cha madiwani amewataka madiwani wa manispaa hiyo kufanya kazi kwa Pamoja wakishirikiana na wataalam ili kuwezesha halmashauri yao kupiga hatua kubwa za maendeleo. Akisoma taarifa ya makisio ya mapato na matumizi ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwantumu Mgonja alisema kuwa halmashauri hiyo inataraia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 37.3  ambapo makusanyo kutoka mapato ya ndani yanakisiwa kuwa shilingi bilioni 4.1 na mapato ya ruzuku kutoka serikali kuu ni shilingi 22.1 bilioni kwa ajiili ya mishahara ya watumishi. Mgonja alisema kuwa katika makusanyo hayo wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 9.9 ruzuku kutoka serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo huku kiasi cha shilingi Bilioni moja kwa matumizi mengineyo (OC).

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI