Header Ads Widget

MAGARI 13 YAKABIDHIWA SEKTA YA AFYA NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBEKutokana na changamoto kubwa ya uhaba wa vyombo vya usafiri katika sekta ya afya na kusababisha adha kubwa kwa wananchi pindi wanapopatwa na tatizo la dharula serikali nchini imelazimika kupeleka gari kila halmashauri ili kukabiliana na adha hiyo.Mkoa wa Njombe umekabidhiwa magari 13 yatakayohudumu kwenye halmashauri zote sita Hospitali na Chuo cha uuguzi kibena ambapo Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary wakati wa kukabidhi magari hayo amesema  yakasaidie kutatua changamoto hiyo.Taarifa ya Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe iliyowasilishwa na Dokta David Ntahindwa imeeleza kuwa magari hayo yatasaidia kuongeza usimamizi katika vituo vya afya na kusafirisha wagonjwa wa Dharula.Ujumbe wa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe ni kwa madereva kuwa makini katika uendeshaji wa vyombo hivyo vya moto huku Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Dokta Frank Mganga akikiri kuwapo kwa changamoto kubwa ya usafiri katika vituo vya kutolea huduma za afya.Akizindua zoezi la ugawaji magari hayo Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ameonya tabia za baadhi ya madereva kuyatumia magari hayo kubeba bangi,kupiga ving'ora bila sababu maalumu pamoja na ulevi utakaosababisha ajali kwenye vyombo hivyo vya moto na kwa raia.Kwa upande wao wananchi mkoani Njombe akiwemo Francis Nindi na Christina Mzena mbali na kushukuru kwa kuletwa kwa magari hayo lakini wanaomba yawe msaada pindi wanapokumbwa na maswaibu ya kiafya huko uraiani.Hadi sasa mkoa wa Njombe katika sekta ya afya una magari 23 yanayoendelea kusaidia wananchi katika suala la ufuatiliaji wa huduma pamoja na kusafirisha wagonjwa[Ambulance].

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI