Na Matukio Daima App,Dar
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (PCCB) mkoa wa Kinondoni imefanya ufuatiliaji na kubaini kampuni iliyopewa jukumu la kukusanya ushuru wa masoko ya Manispaa hiyo imekua ikifanya udanganyinfu katika ukusanyaji na uwasilishaji wa mapato hayo benki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni Ismail Selemani amesema kuwa hatua hiyo imekuja kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo pamoja na ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.
Amesema kuwa, kwa kipindi cha mwezi oktoba na Novemba mwaka 2023 imefanya ufuatiliaji na uangalizi wa kichunguzi kwa muda wa siku 6 na kuthibitisha kuwa kampuni ya Prezidar inakusanya na kuwasilisha benki kiasi kidogo kuliko uhalisia wake.
Aidha, pia imefanya uchunguzi kuhusiana na mapato hayo na kubaini kuwa watendaji wa kampuni kivuhiyo wamekua wakihujumu mapato kwa kutumia POS mashine ipasavyo, hivyo Jan 10, 2024 walishtakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kivukoni.
"Watuhumiwa wote walishtakiwa kwa tuhuma za uhujumu uchumi, ubadhirifu, kusaidia kutenda kosa, kuongoza genge la uhalifu na uchepushaji wa mapato ya ushuru ambapo makosa hayo yalifunguliwa kesi namba 1638/2024"amesema Selemen.
Aidha, amewataka wafanyabishara wote kuzingatia miongozo inayotolewa na halmashauri na Serikali kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru na kuhakikisha wanapatiwa stakabadhi sawa na kiasi walichotoa, huku Halmashauri ikitakiwa kusimamia kwa ukaribu wazabuni wote waliopewa dhamana ya ukusanyaji ushuru kwa niaba ya Halmashauri.
0 Comments