Na mwandishi wetu Matukio app. Mtwara
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mtwara Rose Ally Ebrahim amewataka Wadau wa Mahakama kushiriki katika boreshaji mbalimbali za Mahakama ikiwemo vifaa vya TEHAMA ilikufanikisha kesi za mahakama ya mtandao.
Kauli hiyo ameitoa katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambapo alisema kuwa maboresho hayo yataendana na UPATIKANAJI WA haki na urekebishwaji wa Sheria mbalimbali kupitia taasisi za Sheria na bunge.
Amesema kuwa kutokana na maboresho yaliyofanywa wamejizatiti kupunguza mashauri na kuondoa kero ikiwemo mlundikano.
"Ilikutatua migogoro na kuzuia mlundikano wa mashauri katika Mahakama kwakutatua migogoro Ili kudumisha amani na utulivu na maendeleo ndani ya jamii yetu" alisema Jaji Rose
Nae Mwenyekiti wa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) mkoa wa Mtwara Steven Lekey alisema kuwa Ili kuwa na nidhamu Kwa mawakili hakuna budi kutungwa kwa kanuni zitakazo simamia mawakili.
"Tandahimba Mahakama yetu tukufu kuratibu wadau wa haki ili nakufanyia maboresho ya sheria na kanuni zinazosimamia nidhamu ya Mawakili ilikuwa na misingi bora zaidi ya usimamiaji wa haki za mawakili" Lekey
Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala amesema kuwa wadau wa Sheria wanapaswa kutenda haki katika majukumu yao ambapo wananchi kuijua haki na wajibu wake wanaweza kutii sheria bila shuruti ili amani na utulivu uendelee kuwepo nchini.
0 Comments