HALMASHAURI ya Wilaya ya Busokelo mkoani imepokea kiasi cha Sh. bilioni 12,578,640,411.94 kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwezesha wananchi kiuchumi katika kipindi cha miaka mitatu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Bi.Loema Peter, alisema hayo Januari 31, 2024 wakati akiwasilisha taarifa ya manafiniko ya serikali ya awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitatu katika mkutano wa Waandishi wa Habari na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Wakurugenzi wa Halmashauri uliyofanika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Alisema kutokana na fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Loema alitoa mchanganuo kuwa Katika Hosiptali ya Wilaya, halmashauri ilipokea Sh. milioni 890 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti (mochari), Wodi ya Wanawake, Wodi ya Wanaume, wodi ya Watoto,jengo la upasuaj,ujenzi wa nyumba ya watumishi 3 in 1 ambapo majengo yamekamilika na yanatumika.
Aliongeza kuwa ujenzi wa Kituo cha Afya kifunda kilichopo kata ya Lufilyo, halmashauri ilipokea Sh. milioni 500 kwa ajili ya umaliziaji jengo la wagonjwa wa nje( OPD), Jengo la mama na mtoto, maabara, jengo la kufulia na kichomea taka.
Mkurugenzi huyo alisema fedha hizo zilizopelekwa katika Halmashauri hiyo, oia zimetumika kujenga Zahanati mpya 9 ambazo sasa zimeongezeka kutoka zahanati 20 zilizokuwepo awali na kufikia 29.
Kuhusu viituo vya Afya alisema vilikuwa 4 kimeongezeka kimoja na kuvifanya kuwa vitano pamoja na hospitali moja ya Wilaya ambayo imeshaanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi cha miaka mitatu halmashauri hiyo imetumia Sh. milioni 864.7 za mapato ya ndani kujenga zahanati katika Kijiji cha Nsoso ambayo imekamilika na inatumika, ujenzi wa Bweni la Wavulana katika Shule ya mchepuo wa Kingereza ya Angaza.
Alisema fedha hizo za mapato ya ndani zimetumika kuwezesha Wananchi kiuchumi ambapo vikundi 120 sawa na Wananchi 1,014. walinufaika.
Akizungumzia mafanikio katika sekta ya Elimu Bi. Leoma alisema kuwa katika Idara ya Elimu Msingi zimejengwa shule mbili za msingi mpya na kufanya ongezeko la shule kufikia 64, Sekondari nne mpya zimejengwa na hivyo kufanya idadi ya shule kufikia 22 kutoka 18 zilizokuwepo awali.
Katika hatua nyingine serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya Busokelo Sh. 3,050,000,000 kwa ajili ya ujenzi, wa jengo la utawala ukamilishaji na kuweka samani ambapo utekelezaji umefanyika na jengo linatumika na ununuzi wa samani upo hatua za mwisho muda wowote zinaanza kutumika
0 Comments