NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANANCHI wa kata ya Kibosho magharibi na kata za jirani wanaenda kuondokana na kero ya ubovu wa barabara baada ya serikali kuanza ukarabati wa barabara ya Weruweru - Manushi - Kombo yenye urefu wa kilomita 10.2.
Barabara hiyo ambayo iko katika bajeti ya mwaka wa 2023/2024 iko katika Kata ya Kibosho Magharibi, na kazi ya ujenzi inaendelea.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi kuiomba Serikali kutatua changamoto hiyo.
Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha kubwa na wananchi kurokana na barabara hiyo kupitika kwa tabu hasa kipindi cha mvua.
Aidha walimshukuru Mbunge pamoja na Diwani wa Kata ya Kibosho Magharibi kwa kupigania mradi huu wenye manufaa kwa wananchi wa Kibosho Magharibi.
Mradi huu ukikamilika utaondoa adha kubwa ya usafiiri hususani wananchi wa vijiji vya Kombo, Manushi Ndoo, Sinde na Kata za jirani.
Mkandarasi aliyepewa zabuni hiyo ni Brand Mark Contractor Ltd ambapo wanategemea kukabidhi mradi huo Juni 2 mwaka huu.
Mwisho..
0 Comments