Header Ads Widget

TAARIFA KWA UMMA WA MACHINGA


Tarehe 08.02.2024 nilikamatwa na Polisi kwa tuhuma za uongo ambazo zilitolewa na Zabron Chengula (Zeche) pamoja na Kessy kwa Katibu Mwenezi, itikadi wa Chama Cha Mapinduzi. Kwamba nimekula hela shilingi 25,000,000 ambazo alizitoa MNEC Salim Asas kwaajili ya Machinga Iringa. 


Kwamba nimekaa mahabusu siku 4 mfululizo kwa tuhuma ambazo zinadhaminika na kimsingi ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria, nimekaa mahabusu kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa Halima Dendego, ambapo mawakili wangu na ndugu zangu wengine wakiwepo Machinga kila walipotaka kuniombea dhamana OCCID Alisema swala hili lipo juu ya uwezo wake. 


Kipekee nimshukuru Katibu Mwenezi wa CCM Paul Makonda kwa hatua za makusudi alizochukua kulifuatilia jambo hili ni kubaini kwamba naonewa tu bila sababu za msingi. 


Nawashukuru Sana mawakili wangu wakiongozwa na Emmanuel Chengula kwa kujitoa kupigania haki yangu ya kuwa huru baada ya kujua nimesingiziwa na ninaonewa bila sababu. 


Nawashukuru Machinga wakiongozwa na Yahya Mpelembwa kwa kupaza sauti na kufuatilia kwa ukaribu juu ya uonezi niliofanyiwa


Pamoja na mengine kipekee namshukuru mbunge wa Iringa mjini Jesca Msambatavangu kwa kuacha shughuli za Kibunge na kufuatilia swala hili kwa ukaribu. 


Shukran zangu za dhati nazielekeza kwa Frank John Nyalusi na convo aliyekua ameambatana nae, kwa kuwasilisha jambo langu kwa IGP Camilius Wambura aweze kutoa maelekezo dhidi ya uonezi dhidi yangu. 


Kwa kutambua kwamba nilipokua kituoni alinifuata askari mmoja wa Mkoani kwa maana ya makao makuu ya jeshi LA Polisi Iringa, alinitishia kwamba watanipoteza kwani hapa Iringa sjui wameshapotezwa wangapi, kauli hii naichukulia kwa umhimu mkubwa kwamba jambo lolote baya litakalo nipata basi Jeshi LA Polisi litakua linahusika, kwa kuwa aliyenitishia namjua vizuri kwa sura yake na alinionya tukiwa tunatazamana nikiwa pale mahabusu. 


Na kwakuwa kituo Polisi sio hotelini, ambapo MTU anaweza kukarishwa na akapafurahia, kwa kuzingatia nimekalishwa siku 4 bila sababu za Msingi zifuatazo ni njia ambazo nitazichukua ili kulinda haki zangu za kuishi kwa Uhuru bila bugudha. 


1. Nimewaagiza mawakili wangu kuwaandikia barua za madai Zabron Chengula na Kessy kwa kunichafua na kusababisha nakaa mahabusu siku 4 huku wakijua kwamba walichoeleza ni tuhuma za uongo kwa nia ya kunichafua na kunitesa Mahabusu bila sababu za Msingi huku wakiharibu mfumo wangu wa maisha. Hivyo haki yangu iliyopotea ni lazima irejeshwe. 


2. Endapo tabia hii ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego ataendelea ya kuniweka mahabusu na kunitoa bila sababu za Msingi zaidi ya chuki binafsi na ukizingatia hii ni mara ya pili, sitasita kumshtaki yeye binafsi kwa majina yake kwa kutumia vibaya madaraka yake kinyume na Sheria za tawala za Mikoa, ili nae ajue kwamba cheo chake kinapaswa kutumiwa kwa busara na kufuata misingi ya haki bila kuingiza chuki binafsi alizo nazo dhidi yangu. 


3. Nitasimamia haki ya kufanya biashara ya mchinga yeyote ambaye anatendewa ndivyo sivyo bila kumuonea mtu wala kupepesa macho, kwani hawa nao ni watanzania wanahitaji haki sawa na watu wengine wowote.

Joseph Mwanakijiji

Naibu Katibu Mkuu Machinga Taifa.


Na Afisa mwandamizi wa Machinga Iringa

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI