Header Ads Widget

CHAMA CHA WABUNIFU MAJENGO (AAT)KUWAKUTANISHA WASHIRIKI 600 SEMINA YA UPANGAJI MIJI INAYOKUA, APRIL 9



Na MWANDISHI WETU

ZAIDI ya washiriki 600 kutoka ndani na nje ya nchi wanataraji kushiriki semina maalumu ya uendeleaji na upangaji wa miji inayokua.

Semina hiyo ya siku mbili imeandaliwa na Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT) itafanyika mjini Morogoro kuanzia Aprili 9-10 mwaka huu.

 Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Rais wa AAT, Meck T’chawi, amesea ni semina muhimu kwani inagusa kwa kiasi kikubwa suala la upangaji miji na ujenzi wa nyumba bora zinazo zingatia teknolojia ya sasa na zamani.

Ameeleza, teknolojia ya ujenzi inakua kwa kasi hivyo kuleta mabadiliko ya ukuaji wa miji.

“Semina hii itasaidia kutoa elimu ya namna ya kupanga miji inayobadilika kuringana na teknolojia ya sasa na ya zamani,”ameeleza T’chawi.

Amebainisha kwa hapa Tanzania miji mingi ilipangwa enzi za ukoloni kipindi cha Mjerumani ingawa changamoto ni kutokana na ongezeko la idadi ya watu linalofanya miji hiyo kuonekana kama skwata.

“Tunahitajika kufanya mbinu mbanndala ili sasa maeneo yanayoonekana ni skwata kuyapanga. Tunaweza kuomba wafadhili li kutusaidia kupanga maeneo hayo. Tukitumia wataalamu wetu inawezekana,”amesema.


Katibu Mtendaji wa AAT, Attie Ahmed Ali, ametoa wito kwa wataalamu wote kushiriki semina hiyo muhimu kwani inawapa wigo mkubwa kutumia ukuaji wa teknolojia na taaluma zao.

“Katika kuunga mkono jitihada za Raisa Dk. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii, semina hii pia itakuwa na tukio la washiriki kwenda kutalii katika mbuga ya wanyama ya Mikumi iliyopo Morogoro,”amesema Attie.

Mwenyekiti wa maandalizi wa semina hiyo, Fortunata Msakamali, amesema washiriki watatoka katika nchi za Afrika Mashariki, Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.

“Itashirikisha wabunifu majengo ndani na nje ya jengo, watu wa mandhari, watu wa teknolojia, wasimamizi wa ujenzi, wasimamizi miradi, mipango miji, wahandisi, wakandarasi, waendelezaji majengo, wahadhili na mafundi,”amebainisha. 

Mjumbe wa kamati hiyo, Catheline Joseph, amesema wakadiriaji wa majenzi wananafasi kubwa kuhakikisha gharama zinazotokana na mabadiliko ya miji zinakuwa sahihi kwaajili ya miji salama ya vizazi vilivyopo na vya baadaye.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI