Wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya wamezilalamikia taasisi za serikali ikiwemo Tanesco kwa kuwa kikwazo kwenye masuala ya uwekezaji wa ndani na kupeleka uwekezaji kuwa hafifu na sekta hiyo kuwa ndogo.
Malalamiko hayo yametolewa na wafanyabiashara Mbele ya kaimu Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji TIC katika semina ya siku Moja kwa wafanyabiashara yenye lengo la kutoa fursa mbalimbali za uwekezaji Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania T.I.C Bw Felix John amesema wafanyabiashara wanahitaji kushirikiana nao Ili waweze kutatua changamoto na vikwazo ambavyo wanakutana navyo.
0 Comments