Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka akizungumza mbele ya waziri wa Ujenzi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga
Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amemuagiza meneja wa Tanroads Mkoa wa Njombe kuendeleza ujenzi wa Km 2 za barabara ya lami kila mwaka kutoka Kijiji cha Ujuni hadi Makete mjini ili kuunganisha kipande cha lami Cha Km 7 kilichojengwa.
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo akiwa Kata ya Kitulo kijiji cha ujuni alipozulu na kukagua ujenzi wa barabara ya kutoka Makete hadi Isyonje kwenda mkoani Mbeya Umbali wa Km 36.3
Jephason Nnko Kaimu mkurugenzi wa miradi toka Tanroads pia ameagizwa na waziri huyo kuwachukulia hatua wakandarasi wote nchini wanaokiuka mikataba ya ujenzi huku kampuni ya Avic International inayojenga barabara ya Makete Isyonje Mbeya kutakiwa kupeleka mitambo yote ndani ya wiki tatu.
Awali diwani wa kata ya Kitulo Abely Mahenge ameomba kujengwa kwa barabara hiyo ambayo imekuwa muhimu katika usafirishaji wa viazi mviringo ambavyo vinalimwa kwa wingi katika eneo hilo.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema kata ya Kitulo imekuwa ikizalisha viazi vinavyosaidia makusanyo ya ndani ya halmashauri ya shilingi milioni 700 hivyo ni muhimu kujengwa kwa barabara hiyo.
Kwa upande wao wananchi wa Ujuni wamekiri kuwa kujengwa kwa barabara hiyo Km 7 kwa kiwango cha lami kumewasaidia sana katika kupunguza adha ya usafirishaji mazao yao kwani awali walikuwa wanatumia gharama kubwa.
Hata hivyo Mbunge wa Makete Festo Sanga amesema matumaini yake ni kwa serikali kuendelea kumsaidia kujenga barabara hizo ambazo katika maeneo mengi ujenzi unaendelea.
0 Comments