Katibu tawala wilaya ya Njombe Agatha Mhaiki akipata ufafanuzi wa namna ya kuandaa lishe bora
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali mkoani Njombe imewataka vijana wa kiume na wa Kike kuacha ulimbukeni wa kuzaa na kuacha kunyonyesha watoto kwa madai ya miili yao kuharibika huku akina baba kutotoa matunzo ya watoto jambo linalosababisha udumavu mkubwa.
Kauli hiyo inatolewa na Agatha Mhaiki Katibu tawala wilaya ya Njombe huko Mtwango kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Njombe ambapo amesema vitendo vya ulimbukeni huo unasababisha watoto wengi kukosa lishe bora inayosababisha kuongezeka kwa udumavu.
Kutokana na kiwango cha Juu cha Udumavu Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dokta Juma Mfanga anasema wamelazimika kuanza kampeni hiyo ya siku sita kwa mkoa mzima ili kufikisha elimu ya lishe bora kwa wananchi.
Baadhi ya wanafunzi katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wameweka wazi namna wanavyofahamu maana ya Lishe kutokana na elimu waliyoipata Darasani.
Prisca Apio na Balton Makweta ni wakazi wa Njombe ambao wanasema kukosekana kwa matunzo kwa akina mama Wajawazito na Ulevi ni miongoni mwa visababisha vya Udumavu kwa watoto.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka
Akiwa Lupembe Barazani kwenye ziara ya Waziri wa Ujenzi,Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema ni lazima wananchi wabadilike kwa aina ya ulaji wa vyakula ili kuepukana na changamoto ya Lishe.
Kwa mujibu wa Ripoti ya viashiria vya Lishe nchini,Mkoa wa Njombe unashika nafasi ya pili Kitaifa kwa Udumavu kwa kuwa na Asilimia 50.4 ukiongozwa na mkoa wa Iringa wenye asilimia 56.9.
0 Comments