Header Ads Widget

SPIKA TULIA MGENI RASMI BUNGE BONANZA

Na Hamida Ramadhan Matukio, Daima App Dodoma

SPIKA wa Bunge Dkt Tulia Ackson  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi

Katika Bonanza linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Jamhuri, Jijini Dodoma.

 

Tamasha hilo la michezo na burudani lijulikanalo kama Bunge Bonanza litafanyika jumamosi, Januari 27.2024 kuanzia Saa 12:00 asubuhi hadi Saa 6:00 mchana, huku akibainisha kuwa


Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu bonanza hilo Mhe Festo Sanga Mbunge na Mwenyekiti wa Bunge Bonanza amesema bonanza hilo ni la Kwanza kwa mwaka 2024, kati ya Matatu yatakayofanyika mwaka huu, nambio za BUNGE MARATHON zinazotarajiwa kufanyika Tarehe 13 Aprili 2024.


Amesema bonanza hilo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Benki ya Azania na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benki ya Azania ikiwa ndiye Mdhamini Mkuu.


" Tamasha hili litabebwa na kauli Mbiu isemayo “UTANI WETU, UMOJA WETU,” amesema Mwenyekiti huyo. 


 Aidha amesema Mgeni wa Heshima kwenye Tamasha hili anatarajiwa kuwa Ndg. Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 


Pia amesema,(TBC) Bonanza  litahusisha mechi za Michezo mbalimbali kati ya Wabunge na Watumishi wanaoshabikia timu za Simba Sports Club na Young Africans Sports Club, lina lengo la kuwahamasisha Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge na Wananchi kwa ujumla kushiriki katika michezo, ili kujenga Afya zao, kutoa burudani na pia kudumisha umoja na kujenga mshikamano miongoni mwetu. 


Amebainisha kuwa bonanza hilo litajumuisha michezo mbalimbali kama Mpira wa Miguu; Mpira wa Kikapu; Mpira wa Pete; Mpira wa Meza; Kuvuta Kamba; Pool Table; Kukimbia Riadha, Kutembea mwendo wa haraka; Kucheza Bao; Kucheza Draft; Kurusha Tufe; Kucheza Karata; mchezo wa Darts (Vishale) Kukimbia na Gunia; Kufukuza Kuku; Kukimbia na yai likiwa kwenye kijiko; kushindana kunywa soda na kula chakula kwa haraka na Kukimbia na glasi ikiwa na maji.


"Kama ilivyoelezwa awali, Mdhamini Mkuu wa Bonanza hili ni Benki ya Azania, ambao wamelipia gharama za vifaa vyote vya michezo, zikiwamo Medali,Tracksuits, T-shirts & Kofia kwa washiriki wote, Mipira ya Michezo mbalimbali, jezi za kila Mchezo utakaochezwa kama timu, zikiakisi rangi za utambulisho wa Timu za SSC na Young Africans SC, na hivyo tumekutana hapa pia kwa ajili ya kupokea Vifaa hivyo rasmi, "amesema . 


Na kuongeza "Wadhamini wetu wameandaa Kifungua kinywa kwa ajili ya Washiriki wote na tafrija jioni ya Siku ya Bonanza kwa ajili ya kuufungua mwaka wa Kimichezo wa 2024," Amesema
Amesema jambo lingine mahususi katika Bonanza hili, ni kupandishwa kiwango cha zawadi kwa Mshindi kinara na jumla katika Bananza letu hili, ambapo Kampuni ya ndege ya Qartar Aiways, imetoa fursa ya Tiketi ya Ndege ya Daraja la Business Class kwa Safari ya Nchi yoyote Duniani, kwa wakati atakaopenda kusafiri mshindi huyo ndani ya miezi Sita ijayo/ mwaka huu.


Amesema Viongozi wakuu wa Timu za Simba Sports Club na Young Africans Sports Club wapo pia mbele zenu ili kutoa hamasa ya Bonanza hili, na watakuwepo kesho viwanjani ili kushiriki kikamilifu, hususani kucheza mchezo wa Kabumbu.


" Nitoe wito Kwa Wakazi wa Jiji la Dodoma na Viunga vyake, karibuni Kesho kuanzia saa 1:00 asb katika Uwanja wa Jamhuri ili mjionee Mitanange ya nguvu kati ya Wabunge na Watumishi wa Ofisi ya Bunge wanaoshabikia Timu za SSC na Young Africans SC, tujue nani ni mkali zaidi, " Amesema.
Mkurugenzi Mhazini na Masoko ya Mitaji wa Benki ya Azania Gilbert Mwandamile  amesema Benki hiyo imedhamini bonanza hilo ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya michezo ikiwemo mpira na jezi.


"Benki ya Azania imeona ni vyema watunga sera wadhamini pambano hilo ili wapate fursa ya kujenga mahusiano na makundi mengine kupitia michezo."amesema Mwandamile


Akizungumza kwa niaba ya Timu ya Simba Ally Shatry amewaasa mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi katika pambano hilo huku akisema Simba hawanaga shughuli ndogo.


Kwa upande wake Msemaji na Afisa Habari wa Timu ya soka ya Yanga Ally Kamwe amesema wapo pamoja na timu ya wabunge wanaoshabikia Yanga huku akisema ni furaha kwa Yanga kujumuika kwenye bonanza hilo huku akiwahamasisha wabunge kujipanga na kufanya vizuri katika mpambano huo.


"Kesho tunafunga ofisi Jangwani tunahamia Dodoma ,hatutaki kucheza na mtu ,maana sisi ikishawekwa logo ya Yanga mahali ,shughuli hiyo tunaichukulia kwa umuhimu mkubwa ,kwa hiyo wabunge nendeni mkautwange sisi tupo nyuma yenu."


Mwisho

Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS