Header Ads Widget

SPIKA TULIA AITAKA JAMII KUFANYA MAZOEZI




Na Hamida Ramadhan Matukio, Daima App Dodoma

SPIKA wa Bunge Dkt Tulia Ackson  ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuweza kukabiliana na magongwa yasiyo ambukiza.


Hayo yameelezwa leo January 27,2024 jijini Dodoma katika tamasha la michezo na burudani lililojulikana kama Bunge Bonanza litafanyika lililofanyika katika Viwanja vya Jamhuri, Dodoma amesema kufanya mazoezi ni sehemu ya kuifanya jamii kuepukana na magongwa yasiokuwa yakuambukiza amabayo yamekuwa yakiupa mzigo mkubwa serikali kukabiliana nayo.


Bonanza hilo liliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Benki ya Azania na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,huku Benki ya Azania ikiwa ndiye Mdhamini Mkuu.


Amesema suala zima la ufanyaji wa mazoezi liliwekewa mkazo na Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambapo alisisitiza umuhimu wakifanya mazoezi kwa viongozi na jamii kwa ujumla. 


"Hivyo basi kutokana na wito huo wa kujitoa na kufanya mazoezi Sisi kama viongozi wenu tumeona tuonyeshe kwa vitendo ili jamii yetu nayoifuate, " Amesema 


Amesema bonanza hilo ni la Kwanza kwa mwaka 2024, kati ya Matatu yatakayofanyika mwaka huu, nambio za BUNGE MARATHON zinazotarajiwa kufanyika Tarehe 13 Aprili 2024 ambapo mwaka huu litakuja kivingine kila mbunge atakimbia na wananchi wake.


 Festo Sanga Mbunge na Mwenyekiti wa Bunge Bonanza amesema bonanza hilo ni la Kwanza kwa mwaka 2024, kati ya Matatu yatakayofanyika mwaka huu, nambio za BUNGE MARATHON zinazotarajiwa kufanyika Tarehe 13 Aprili 2024.


Amesema Azania Benk wamejitoa kudhamini bonanza huku akiahidi kuwa wateja kwa shughuli mbalimali za kifedha. 


Pia amewashukuru viongozi wa Timu ya Simba na Yanga kwa kushirikiana pamoja huku wengine wakishiliki katika michezo hiyo iliyoandaliwa kwenye bonanza Hilo. 



Katika tamasha hilo umepigwa Mchezo wa Bunge Bonanza ambapo wabunge wanaoishabikia Yanga walicheza mchezo na wabunge wanaoshabikia Simba na kwa upande wa Mpira wa Miguu Yanga wameendeleza ubabe


Aidha Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku bao la Yanga likifungwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na kupelekea mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati


Wabunge wanaoishabikia Yanga waliwaadhibu wabunge wanaoishabikia Simba kwa kupata ushindi kupitia mikwaju ya penati


Tamasha hilo limebebwa na kauli Mbiu isemayo “UTANI WETU, UMOJA WETU,” amesema Mwenyekiti huyo. 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI