NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Zaidi ya watu 335 wamekatwa na jeshi la polisi Mkoa hapa huku 133 wakiwa wamehojiwa na kufikishwa mahakamani na wengine 202 wanaendelea kufanyiwa mahojiano pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani Kwa hatua zaidi za sheria
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani hapa Wilbrod Mtafungwa ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya jeshi hilo kufanya misako dhidi ya watu wanaojihususha na matukio ya kiuhalifu .
Mtafungwa amesema kuwa miongoni mwa vielezo vilivyokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na simu za mkononi aina mbalimbali zaidi ya 50, Dawa za kulevya aina ya mirungi, misokoto ya bangi na vifaa vya kufanyia uhalifu pamoja mali zilizoibiwa katika makazi ya watu.
"Taarifa kuhusu uhalifu na waahalifu zimeendelea kupatikana kutokana na ukusanyaji wa taarifa zilizojificha zinazohusu wahalifu kazi inayofanywa Kwa weledi na askari wetu " Amesema Mtafungwa.
Amesema kuwa wamekuwa walipata taarifa kutoka wananchi wasiopenda kuona uhalifu unafanyika hivyo kupitia ushirikishaji wa jamii unaofanywa na jeshi la polisi kupitia mikutano mbalimbali inayoendelea kufanyika katika kata wameweza kupata mafaniko makubwa katika kiwafichua wahalifu katika mitaa.
Aidha Mtafungwa amewataka wananchi kuendelea kufichua matukio ya kihalifu katika jamii ili waweze kuwa hukulia hatua za kisheria dhidi ya watakao bainika wakifanya vitendo hivyo vya kihalifu.
0 Comments