Header Ads Widget

PROF NDAKIDEMI ..'HAPPY BIRTHDAY DKT SAMIA'

Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP, Moshi

Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi ni miongoni mwa viongozi waliojitokeza katika kumtakia heri na baraka tele katika kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan hii leo januari 27 


Prof Ndakidemi amesema kuwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa na upendo wa kipekee kwa watanzania kutokana na mambo mbali mba ya kimandeleo aliyoyafanya kwa kipindi kifupi cha uongozi wake.


'Kiukweli ni lazina niungane na watanzania wenzangu katika kumtakia heri ya kumbukizi kwa rais wetu mpendwa na kumuombea kwa Mungu azidi kumlinda ampe maisha marefu'anasema Prof Ndakidemi

Anasema kwa upendo ambao Dkt Samia ameuonyesha sii tu kwa watanzania bali kipekee kwa upande wa jimbo la Moshi Vijijini wakazi wa jimbo hilo wapo naye katika siku hii muhimu kwake lakini zaidi katika mambo.


Kwa upande wake mkazi wa Kibosho Kirima Ambrose Mushi amesema hana budi kuungana na watanzania wengine kumtakia rais maisha marefu na afya njema


'Namtakia afya njema lakini pia maisha marefu yenye baraka na mafanikio tele hakika Mungu wetu ni muaminifu'anasema


Inyasi Mushi diwani wa Kibosho Kirima naye anasema Mungu azidi kumtunza rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na upendo wake aliouonyesha kwa watanzania.


'Tumepata kiongozi mwenye upendo kwetu kama taifa Mungu amzidishie miaka mingi hapa duniani'

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI