Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP,Moshi.
Baadhi ya viongozi mbali mbali na wananchi wilayani Moshi wameungana na watanzania wengine kumtakia heri na fanaka katika siku hii ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima ni miongoni mwa viongozi waliotuma salam hizo za pongezi kwa rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa.
'Kipekee niungane na watanzania wenzangu katika kumtakia rais wetu ambaye pia ni mwenyekiti wetu heri ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake'
...Mwenyezi Mungu amlinde na kumpa miaka Mongi yenye heri hapa duniani ili aweze kutuongoza vyema kama lilivyo kusudio la Mungu 'happy birthday'anaeleza mwenyekiti huyo
Anasema kipekee kama watanzania tunao wajibu wakuendelea kumuombea rais wetu ili aweze kuongoza taifa na kulifikisha katika nchi ya ahadi kama mwanzo wake ulivyoanza kuonekana.
Kada wa chama cha mapinduzi(CCM)Wakili Emmanuel Mlaki katika mtandao wake wa kijamii wa x ameungana na watanzania wengine kumpongeza mh rais DKT Samia Suluhu Hassan katika siku hii muhimu kwake ambayo ni kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Diwani wa kata ya Njiapanda Loveness Mfinanga amemtakia rais afya njema na kumuombea kwa Mungu azidi kumpa miaka mingi hapa duniani kwani wema wake hautafutika.
'Hakika ametutendea mema kama taifa lakini hata katika kata yangu kaniletea miradi mingi hakika Mungu aendelee kumtunza tunayo hazina kama taifa'anasema
0 Comments