meneja wa Mkoa Afisa Rasilimali watu wa Mkoa Bi Frida Barankena akimlisha mtoto wa kituo Cha Huruma Center
Meneja wa Tanesco mkoa wa Iringa Dotto Chacha akizungumza na wafanyakazi wa Tanesco
TANESCO IRINGA YASOGEZA TABASAMU KENYE KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU CHA HURUMA CENTRE
27 Julai 2024
Na Juma Msuya
Uongozi wa TANESCO Mkoa wa Iringa ukiongozwa na Meneja wa Mkoa Mhandisi Dotto Chacha umesogeza tabasamu la kuendeleza furaha kwa jamii ikiwa ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha mwaka mpya wa 2024, matukio yafuatayo yamefanyika siku hiyo:-
1:Kutoa zawadi ya vitu, vifaa na vyakula mbalambali
2:Kuweka umeme kwenye mita tatu za Mabweni ya kulala watoto ya Huruma Centre
3: Kufanya usafi maeneo mbalimbali ya Kituo
4: Kununua mahitaji, kupika na kushiriki chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu
5: Kutoa elimu ya huduma mbalimbali zilizolenga kujenga mahusiano mema ya watoto, wafanyakazi wa kituo na watumishi wa TANESCO.
📍 Tukio hilo limehusisha michango iliyochangwa na wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Iringa na wilaya zake
📍Akikabidhi zawadi hizo kwenye kituo kwa niaba ya meneja wa Mkoa Afisa Rasilimali watu wa Mkoa Bi Frida Barankena alisisitiza kuwa kazi hii ya kurudisha kwa jamii ni endelevu ikiwemo kushiriki kwenye matukio mengine yanayohusu jamii haswa upandaji wa miti ili kuendelea kuboresha mazingira.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano na Huduma kwa wateja
Mkoa wa Iringa
0 Comments