Changamoto ya ubovu wa miundo mbinu ya Barabara katika maeneo Mbali Mbali ya Mji wa Iringa imeendelea kuwatesa wananchi wanaotumia vyombo Vya moto wakiwemo wananchi wa kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa.
Eneo la Mkimbizi katika Manispaa ya Iringa linatajwa kuwa ni eneo lenye Barabara mbovu zaidi ndani ya Manispaa ya Iringa japo ni eneo lililopo ndani ya Manispaa.
Wakazi wa kata ya Mkimbizi ni kama ilivyo kwa wakazi wa kata ya Mwangata na maeneo mengine ambao wamekuwa walilalamikia ubovu wa miundo mbinu Kila uchwao .
Ombi la wananchi kwa Wenye dhamana ya miundo mbinu kuchukua hatua za haraka kufanyia kazi changamoto hizo zinazotesa wananchi na hata kukwamisha shughuli za uzalishaji Mali.
Mapema asubuhi ya Leo kutokana na mvua zinazonyesha wakazi wa Mkimbizi Bima ambao walikuwa katika msafara wa mazishi wamejikuta wakikwama kuendelea na safari baada ya Barabara kuharibika kupita kiasi .
Matukio Daima media tunajiuliza hivi meneja wa TARURA wilaya ya Iringa yupo kazini? anaziona kero hizi ambazo wananchi wanazipata ama anagonja madhara makubwa yatokee ndipo atatue changamoto hizi kwa kufanya kazi usiku na mchana?
0 Comments