Umoja wa wanachama wa Millenium Women Group unaoundwa na wake wa Viongozi umetoa msaada wa taulo za kike (Pad) 400 zenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 1.4 kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Izazi Katika Jimbo la Isiman wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Wake hao wa Viongozi wametoa msaada huo kama Njia ya kuunga mkono jitihada za kumwezesha mtoto wa kike Kusoma Kwa Raha darasani siku zote za masomo pasipo kukosa Kwa kukosa Pad.
"Msaada huu ni Kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa kike asiache kwenda shule kwa siku atakazokuwa kwenye hedhi tunatambua mchango mkubwa ambao Serikali yetu chini ya mama yetu kipenzi Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambayo anaifanya Katika kujenga shule Bora na kumsaidia mtoto wa kike kupata elimu Bora"
Hivyo wao kama wake wa Viongozi Katika kuunga mkono jitihada za Serikali Kwa kuendelea kutoa elimu Kwa watoto wa Kitanzania wakiwemo watoto wa kike wamelazimika kuchangishana pesa na kusaidia Pad hizo ili kumwezesha mtoto wa kike Kusoma Kwa uhuru zaidi .
Wake hao wa Viongozi wametoa Msaada huo kupitia mwanachama Mwenzao Germina Lukuvi ambae ni MKE wa mbunge wa Jimbo la Isimani mhe Wiliam Lukuvi ambae pia ni Mshauri wa mheshimiwa Rais Dkt Samia .
MKUU WA SHULE AMELYE LONGOkwa upande wake mkuu wa Shule hiyo Amelye Longo mbali ya kuwashukuru wanachama hao umepongeza jitihada Kubwa za kimaendeleo zinazofanya na mbunge Lukuvi jimboni Isiman ikiwa ni pamoja na Moyo wake wa kujitoa Kwa ajili ya wana Isiman hata kuendelea kuwakumbuka wanafunzi wa Jimbo la Isimani Kwa kuunga mkono Kwa ujenzi wa Hosteli kwenye shule za Jimbo lake.
Mhe .Wiliam Lukuvi mbunge wa Isiman
Kuwa ni wazi mheshimiwa Lukuvi ameendelea Kuupiga Mwingi na kuwa chachu ya maendeleo ya Jimbo la Isiman.
"Kwa niaba ya jumuiya ya Izazi tunawashukuru sana Kwa Moyo wenu wa kusaidia jamii. Kwa hakika nimeona namna watoto wa kike walivyofurahi kupewa taulo za kike. Tunaomba utufikishie shukrani Kwa MILLENNIUM GROUP Kwa Nia njema hii Kwa mtoto wa kike Jambo hili kinapunguza sana Utoro wa rejareja Kwa wanafunzi"alisema Longo
0 Comments