Header Ads Widget

FLAVIANA MATATA AKABIDHI MATUNDU 12 YA VYOO MANYUNYU SEKONDARI NJOMBE.

 






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Waziri wa elimu nchini Tanzania Profesa Adolf Mkenda ameagiza utunzwaji wa miundombinu ya elimu inayojengwa na serikali pamoja na wadau wengine wa elimu kwani mazingira rafiki huwafanya wanafunzi kusoma kwa utulivu mkubwa.


Agizo la Waziri wa Elimu linatolewa baada ya Taasisi ya Flaviana Matata Foundation kukabidhi mradi wa matundu ya vyoo 12 yaliyokamilika katika shule ya sekondari ya Wasichana Manyunyu iliyopo kata ya Matembwe Wilayani Njombe kwa lengo la kupunguza  changamoto ya uhaba wa vyoo  katika shule hiyo.


Akizungumza kwa njia ya simu Prof.Mkenda aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Elimu Maalum Tanzania Dkt. Magreth Matonya ameipongeza taasisi hiyo kwa kuunga juhudi za serikali katika kutatua changamoto ya miundombinu katika sekta ya Elimu.


Kwa upande wa Dkt. Magreth Matonya Mkurugenzi wa elimu Maalum toka wizara ya Elimu ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa iliyoifanya huku akiwataka wanafunzi kukazana katika masomo yao ili wazifikie ndoto zao.


Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation,Flaviana Matata amesema lengo la mradi huo ni kuweka mazingira salama kwa watoto wa kike hasa wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.


Awali Katibu Tawala wilaya ya Njombe Agatha Mhaiki ametumia fursa hiyo kuishukuru Taasisi ya Flaviana Matata kwa kujenga vyoo hivyo huku akiwaonya wanafunzi kutojiingiza kwenye makundi yatakayowahiribia maisha yao.


Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Manyunyu akiwemo Philipina Mbatina anayesoma kidato cha tano amesema vyoo hivyo vinaenda kutatua changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI