Header Ads Widget

DC WA KILOMBERO DUSTAN KYOBYA AMEIFUNGUA RASMI SHULE MPYA YA SEKONDARY LIPANGALALA

 


Na Mwl. Kassim Mandwanga

Kidatu Kilombero 

  Mkuu wa wilaya ya Kilombero Dustan Kyobya na  mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Kilombero, ameambatana na viongozi kadhaa wa halmashauri katika zoezi la ufunguzi wa shule mpya ya sekondari Lipangalala.


 DC Kyobya alikuwa ameongozana na Mkurugenzi wa halmashauri comrade Zahra Michuzi, Mh Kassim Faya  Nakapala mwenyekiti wa halmashauri, Comrade Mwambeleko katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya pamoja na afisa elimu sekondari ndugu  Godwin Samson Mukaruka.



Sambamba na ufunguzi huo Kyobya alipanda mti wa kumbukumbu na  kusisitiza mambo yafuatayo:


 mkuu wa wilaya amesisitiza kutunzwa kwa  miundombinu ya shule hiyo kwa kuwa ndoto ya wana Kilombero ni kuona shule hiyo inakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita.


Katika swala la lishe mkuu wa wilaya amewakumbusha wazazi kizingatia muongozo wa elimu bila malipo kwamba mzazi ana jukumu la kumpatia chakula mtoto, hivyo basi amewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni hapo.


DC, ambaye ni mtu wa vitendo sana, akasisitiza pia majengo yaliyosalia yakamilishwe kabla ya tarehe 22 January 2024.



Sambamba na hilo mwenyekiti wa halmashauri cde Kassim Faya Nakapala ambaye pia ni diwani wa kata ya Lipangalala  amemshukuru sana Mh DC na Mkurugenzi kwa utendaji wao wa kazi wa viwango vya juu na kwamba utendaji huo umekuwa chachu ya ukamilikaji wa shule hiyo uliokwama kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu.


Mwenyekiti huyo pia amewashukuru wananchi na kuwataka wanafunzi kusoma Kwa bidii


Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kilombero cde Mwambeleko amewataka wananchi kuwa na imani na Mh Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali yake, pia amewapongeza Mh DC na Mkurugenzi Kwa utendaji wao mzuri pamoja na kuwataka wanafunzi kusoma Kwa bidii.

#Uzalendo ni vitendo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI