Header Ads Widget

ZITTO AWATAKA POLISI WASITUMIE NGUVU KUZUIA 'KAMCHAPE'

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kalinzi  Kigoma Vijijini  mkoani Kigoma
Na Fadhili Abdallah, Kigoma

 


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameitaka polisi mkoa Kigoma kuacha kutumia nguvu katika kushughulikia suala la kutoa uchawi kwa wananchi kwenye nyumba za watu kunakofanywa na kikundi cha waganga wa jadi maarufu kama kamchape badala yake elimu itumike kushughulikia jambo hilo.

 

Zitto alisema hayo akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Kalinzi Kigoma Vijijini ambapo alisema kuwa matumizi ya nguvu yameleta madhara makubwa kwa wananchi badala ya kuwa suluhu ya jambo hilo.

 

Alisema kuwa wananchi wameingia Imani kubwa ya kuwepo kwa watu hao (Kamchape) jambo linalowapa nguvu waganga hao kuendelea na jambo hilo hivyo polisi kutumia nguvu na kusababisha mauaji haitaweza kulimaliza jambo hilo.

 

“Hatuungi mkono vitendo vya kamchape vinavyoendelea lakini haitawezekana kutatua jambo hili la kijamii kwa kutumia nguvu za jeshi tayari wapo watu wameuawa na mali kuharibiwa, ni vizuri polisi wakakabidhi jambo lishughulikiwe kijamii na elimu ikatolewa kwa wananchi kuwaelewesha madhara ya kuunga mkono vitendo hivyo,” Alisema Zitto

 

Waziri kivuli wa mifugo na uvuvi ACT Wazalendo Kiza Mayeye akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Kalinzi Kigoma Vijijini

Awali Waziri Kivuri wa mifugo na uvuvi ACT Wazalendo, Kiza Mayeye ameitaka serikali kuanzisha soko la kahawa mkoani Kigoma badala ya wakulima hao kubeba kahawa yao na Kwenda kuuza Moshi mkoani Kilimanjaro.

 


Mwisho.

Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS