Header Ads Widget

TCRA YATOA ELIMU KWA WAKUU WA SHULE ZANZIBAR

 

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar imetoa elimu kuhusu Uanzishwaji na Uendeshaji wa Klabu za Kidijiti kwa Wakuu wa Shule za Sekondari Zanzibar (JUWASEZA) kwenye kikao kazi kilichofanyika kisiwa cha Pemba.


Meneja wa Mamlaka hiyo Ofisi ya Zanzibar, Esuvatie Masinga, akizungumza mara baada ya utoaji wa elimu hiyo, alisema Wakuu wa Shule za Sekondari ni msingi muhimu katika kuhakikisha Klabu za Kidijiti zinaanzishwa kwenye skuli na kuendeshwa ili ziwanufaishe wanafunzi kuwa washiriki kamili katika kujenga uchumi wa kidijiti na buluu.


“Ushiriki wa vijana kwenye uchumi wa kidijiti na buluu ni wa msingi sana; hii ndiyo sababu tumeazimia kuwafikia wanafunzi kupitia wakuu wa shule kwa kuwa wanayo nguvu ya ushawishi kama Viongozi watakaochagiza Uanzishaji wa klabu hizi muhimu,” alisema.


Aidha alisema kuwa ili kujenga uchumi wa kisasa unaoegemea zaidi matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, ushiriki wa vijana ni muhimu sana.

“Vijana ndiyo nguzo muhimu ya kuimarisha na kujenga uchumi wa kidijiti, lengo letu ni kuhakikisha vijana wanajiunga na kuwa washiriki wa Klabu za Kidijiti zitakazowapatia maarifa ya teknolojia kupitia masomo ya STEM yaani Hisabati, Sayansi, Teknolojia na Uhandisi,”


Alifahamisha kuwa TCRA itaendelea kuhamasisha ubunifu na uvumbuzi katika klabu za kidijiti zilizoanzishwa na zitakazoanzishwa ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo waratibu wa klabu za kidijiti ili waweze kuzisimamia vyema ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.


Hivyo, alisema, wataendelea kutoa elimu kwa shule mbalimbali ili kuona elimu hiyo inawafikia wananchi waliokuwa wengi.


Aidha alisema TCRA taendelea kushirikiana na wakuu wa shule kwani wataweza kusadia uanzishwaji wa Klabu nyengine za masomo ikiwemo Klabu za Hisabu, Kiiengereza.

Sambamba na hayo, alisema, ili tujenge uchumi wa kidijiti na buluu matumizi ya TEHAMA hayaepukiki hivyo ni TCRA itaendelea kuwaandaa vijana.


Sambamba na hayo, aliwaasa wanafunzi pamoja na walimu ambao ni walezi kujiunga kwenye klabu za kidijiti kwa kujisajili moja kwa moja kupitia tovuti ya https://digitalclubs.tz au kuzianzisha moja kwa moja katika skuli zao kwa kupata utaratibu wa uanzishaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUWASEZA, Khatibu Rashidi ,aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Ofisi ya Zanzibar kwa kuona umuhimu wa kuwapa walimu wakuu Elimu ya Uanzishaji wa Klabu za Kidijiti ambazo zitakuwa zenye mchango mkubwa katika kuwahamasisha wanafunzi kuifahamu zaidi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.


“Hakika tumefaidi sana kwa semina ambayo mmetupatia, huu ni msingi mzuri wa kuwajengea uwezo wanafunzi wetu hasa tutakapoanzisha klabu hizi kwenye shule zetu,”alisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI