Header Ads Widget

KIZA MAYEYE AJITOSA KUGOMBEA UENYEKITI ACT KIGOMA

 

Kiza Mayeye Waziri Kivuli Mifugo na Uvuvi ACT Wazalendo amechukua fomu kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho mkoa Kigoma

Mwenyekiti wa Chama cha ACT   jimbo la Kasulu mjini ,Haruna Kwasakwasa (kushoto)  akipokea  fomu ya kugombea nafasi  ya Mwenyekiti wa chama hicho mkoa Kigoma kwa niaba ya Waziri Kivuli wa mifugo na Uvuvi Kiza Mayeye ambaye ameonesha nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Chama cha ACT Wazalendo mkoa Kigoma.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzo ACT Wazalendo mkoa Kigoma Juma Ramadhani akizungumza katika siku ya kwanza (uzinduzi) wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ndani ya chama hicho


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHAMA chaa ACT Wazalendo leo  kimezindua mchakato wa uchaguzi wa ndani kwa ajili ya kuwapata viongozi wake wa ngazi ya mkoa ambapo mkoani Kigoma Waziri Kivuli wa mifugo na Uvuvi wa chama hicho Kiza Mayeye amejitokeza kuchukua fomu kwa ngazi ya nafasi ya uenyekiti wa ACT mkoa Kigoma.

 

Zoezi hilo limezinduliwa rasmi na Katibu wa ACT Wazalendo mkoa Kigoma, Juma Ramadhani ambaye alisema kuwa uchukuzi wa fomu kwa ngazi mbalimbali za uongozi mkoani humo zimeanza kutolewa leo Desemba 28  hadi Januari 9 mwakani zoezi litakapofungwa kusubiri uchaguzi utakaofanyika Januari 12 mwakani.

 

Ramadhani ambaye Ni Mwenyekiti wa uchaguzi wa chama cha ACT Wazalendo mkoa Kigoma alisema kuwa kwa nafasi ya Mwenyekiti wa mkoa na ngome za vijana, wazee na wanawake fomu zitatolewa kwa kiasi cha shilingi 10,000 ambazo zitalipwa benki kwa kupitia akaunti ya chama hicho mkoa Kigoma.

 

Katika uzinduzi huo wa uchukuaji fomu Waziri Kivuli wa mifugo na uvuvi ACT wazalendo, Kiza Mayeye amejitokeza kuchukua fomu kwa nafasi ya uenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa Kigoma ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho jimbo la Kasulu,Haruna Kwasakwasa alichukua fomu hiyo kwa niaba ya kiongozi huyo.


Akizungumza baada ya kuchukua fomu kwa niaba ya Kiza Mayeye  mwenyekiti huyo wa jimbo la Kasulu alisema kuwa anatimiza katiba ya chama na demokrasi ya chama hicho akiamini kuwa Mayeye anao uwezo mkubwa wa kukivusha chama hicho mkoani Kigoma.


Wengine waliojitokeza kuchukua fomu kwenye uzinduzi huo ni pamoja na Diwani wa viti maalum Manispaa ya Kigoma Ujiji, Tatu Amani ambaye amechukua fomu kugombea nafasi ya Mwwenyekiti wa ngome ya wanawake.


Afisa Uchaguzi wa ACT mkoa Kigoma, Azizi Ally alisema kuwa kuanzia Desemba 28 mwaka huu hadi Januari 9 fomu zitakuwa zikipatikana kwenye ofisi za majimbo kwa wale wa wilayani na ofisi ya mkoa itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni kwa kipindi chote cha uchukuaji fomu kilichotangazwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI