Header Ads Widget

TANZANIA NA MALAWI WATILIANA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO BANDARI YA DAR


Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 

Tanzania na Malawi zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano kuhusu ushoroba wa kusafirishaji baina ya nchi hizo mbili huku ikielezwa Malawi itatumia Bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo wa ushiriakino wa ushoroba wa usafirishaji, Waziri Profesa Mbarawa amesema mkataba huo utakua na faida kwa nchi zote mbili ambapo Tanzania ndio watakua wanufaika wakubwa kwani nchi ya Malawi imtumiaji wa bandari ya Dar es Salaam.


Aidha, amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita imefanya maboresho makumbwa kwenye bandari ya Dar es Salaam kuanzia gati namba moja hadi namba saba huku akifafanua kuwa wamejenga gati maalum kwa ajili ya gati namba zero.


"Kwa kuwa mkataba huu ulikuwa wa muda mrefu tumeweza kusaini upya kwa lengo la kuhakikisha kwamba sasa unafanya vizuri zaidi, Serikali imejenga miundombinu mingi kwa ajili ya kuboresha ushoroba huo wa usafirishaji kati ya nchi hizo mbili, " amesema.


Ameongeza kuwa katika kuendelea kupanua uwezo wa bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha utoaji huduma ndio maana wameamua kutoa nafasi kwa sekta binafsi kufanya uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kusisitiza wanafanya hayo yote kuhakikisha wanaongeza ufanisi kwa ajili ya bandari hiyo.



Hata hivyo, amesema Serikali imefanya mabadiliko makubwa ikiwemo kujenga gati la kisasa mbali na urefu takribani mita 300 inafanya kazi na wameweka vifaa vya kisasa.


Amesema kuwa, mkataba huo unafaida kwa Tanzania na Malawi huku akieleza kwamba kwa mwaka 2022 mzigo ulihudumiwa na bandari ya Dar es Salaam kwa nchi ya Malawi ulikuwa takribani ya zaidi tani 500, 000


"Lakini ukilinganisha na mwaka 2018 kumekuwa na ongezeko kubwa hivyo tunataka ongezeko lifikie hadi tani million moja au mbili na hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam


"Tumekuwa tukisaini mikataba kwa ajili ya kuifungua Bandari ya Dar es Salaam japo kuna ushindani na tukipanga vizuri kama tunavyoendelea na ujenzi wa miundombinu hakuna mtu ataweza kushindana. Kwenye bandari ya Dar es Salaam.


Hata hivyo, amesema wiki inayokuja wanatarajia kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay ambayo ni muhumi kwa wakazi wa Ziwa Nyasa.


"Bandari hii ni muhimu kwa ajili ya watu wa Malawi na jitihada zote zinafanywa kuhakikisha wanafungua ushoroba huo kati ya Tanzania na Malawi, ambapo utarahisisha upatikanaji wa bidhaa kwa nchi yao wakitumia korido ya Mtwara ambayo itapunguza gharama ya usafirishaji bidhaa na hivyo wananchi kupata bidhaa kwa bei nafuu.


Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi na Kazi za Umma nchini Malawi  Jacob Hara ametumia nafasi hiyo kuelezea manufaa ambayo yanakwenda kupatikana kwa nchi zote mbili baada ya kusaini mkataba huo unaotoa fursa kwa nchi yao kutumia bandari ya Dar es Salaam.


Aidha amesema anaamini mkataba huo waliousaini utasaidia kufanya kazi kwa pamoja kati ya Tanzania na Malawi na kurahisisha katika sekta ya usafirishaji

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI