Bodi ya Utalii Tanzania, Ofisi ya kanda ya Kusini kwa kushirikiana na wadau wa Utalii imeanza kampeni yake maalumu ya kuhamasisha utalii wa ndani. Kampeni iliyopewa jina la ROYAL TOUR CHRISTMAS MBUGANI yanye lengo la kuhamasisha utalii wa ndani hususani katika msimu huu wa sherehe za siku kuu ya CHRISTMAS.
Kampeni hiyo inaratibiwa Bodi ya Utalii ofisi ya kanda ya kusini kwa kushirikiana na kampuni ya Utalii ya Bateleur tour and Safaris, kampuni ya Mkuta travel na kampuni ya UPL SAFARIS zimeandaa vifurushi maalumu vya utalii ( Tour packages) katika sehemu mbali mbali za vivuti
o vya utalii kama vile Hifadhi ya Taifa Ruaha, Hifadhi ya milima ya Udzungwa, Mpanga kipengere pamoja na maeneo ya kihistoria ya kalenga/Mkwawa Museum na Isimila stone age site.
"Kampeni hii ni mahususi haswa katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii, tunataka tuone watanzania na wanakusini kwa ujumla wanajitokeza kwa wingi katika kampeni hii maalumu na wanatembelea vivutio vya utalii vya kusini katika msimu huu wa likizo na sherehe za Christmas pamoja na mwaka mpya.
Na hii ni kuunga mkono jitihada za alizozoanzisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kampeni yake ya Tanzania The Royal tour"
Nimatarajio yetu kama Bodi kuwa wanachi watajitokeza kwa wingi na kufurahia kwa pamoja katika moja ya vivutio vinavyopatikana kusini mwa Tanzania
Aidha kwa mawasiliano unaweza kuwasiliana na Ofisi ya Bodi ya Utalii ofisi ya Kanda kusini kupitia namba za simu 0715088871 au kupitia Ukurasa wetu wa mitandao ya kijamii @utalii_kusini.
0 Comments