Header Ads Widget

SPIKA WA BUNGE : WAKULIMA WA MVIWATA ONGEZENI UBORA WA MAZAO ILI YAPATE SOKO LA KIMATAIFA.

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa mabunge duniani IPU  Dkt.Tulia Akson  amewataka Wakulima nchini kuendelea kuzalisha na kupandisha thamani mazao  yao kwani  kufanya hivyo kutapanua soko la  kimataifa na kuwa na uhakika na kilimo.

Dkt.Tulia Akson  amesema hayo Mkoani Njombe katika ufunguzi wa mkutano wa 28 na maadhimisho ya miaka 30  ya Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania MVIWATA  uliokutanisha wakulima wadogo kutoka mikoa ya  Tanzania na nchi mbalimbali  ambapo amesema ni wakati muafaka sasa  kwa wakulima kuongeza tija ya uzalishaji Ili kulisha taifa mara dufu.


Antony Mtaka ni mkuu wa mkoa wa Njombe amewataka watanzania ambao  ni wakulima ,licha ya kuzalisha mazao kwa wingi wakumbuke kuwaandalia watoto wao   chakula ambacho kimeongezwa virutubisho.

Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA Tanzania  Stephen Ruvuga akizungumza katika mkutano huo ameiomba serikali kuweka mazingira rafiki kwa wakulima wadogo ili waweze kuongeza tija katika sekta ya kilimo kwani endapo mifumo bora itawekwa itapunguza changamoto ya kupungua kwa chakula nchini.

Ruvuga pia ameomba kushughulikiwa kwa changamoto ya soko la mazao mbalimbali kwani wakati mwingine bei ya mazao imekuwa mwiba mkubwa kwa wakulima ukilinganisha na gharama ya mbolea.

 

Kilio cha Wakulima Mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Akson Ambaye Ndiyo Mgeni wa heshima  Katika Mkutano Huu ameiomba Serikali Kulichukulia Suala Hilo Kwa Uzito.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI