Header Ads Widget

KAMPUNI YA KUONGOZA WATALII YA AFRICAN SCENIC SAFARIS KUFANYA MAANDALIZI YA TWENZETU KILELENI 2024.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 

MKURUGENZI wa kampuni ya kuongoza watalii ya African Scenic Safaris, Simbo Natae amasema kuwa kampuni yake hiyo itaanza maamdalizi mapema ya kampeni ya Twenzetu Kileleni ya mwaka 2024 kuathimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika ili kupata Watanzania wengi. 


Kampuni hiyo ya kuongoza watalii kwa mara ya kwanza mwaka huu imeaminiwa na Hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), na kukabidhiwa njia ya Lemosho kupeleka wageni katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika. 


Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maandalizi ya Twenzetu Kileleni 2024, Natae alisema kuwa, hii ni kwa mara  ya kwanza wanashiriki kampeni hiyo hivo wamejifunza na kuahidi kuanza maandalizi mapema ya mwakani ili kupata wageni wengi watakaopanda mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Lemosho. 


"Ni kwa mara ya kwanza njia hii ya Lemosho inapandisha wageni kupitia kampeni ya Twenzetu Kileleni inatumika kuwapeleka wageni katika kilele cha mlima Kilimanjaro na imekuwa ni kwa kampuni yetu tunajivunia kuaminiwa na KINAPA" Alisema Mkurugenzi Natae. 


Na kuongeza "Njia hii ni mahususi kabisa na njia bora ya kupanda mlima Kilimanjaro ndio maana wageni wote waliotumia njia hii wamefanikiwa kufika kilele cha Uhuru na kurudi salama".


Alisema kuwa, kupitia njia hiyo ya Lemosho inawasaidia wageni kuviona vilele vyote vitatu vya mlima Kilimanjaro ambavo ni Shira, Kibo na Mawenzi ambapo hutumia siku 8 mpaka kufika kileleni na kurudi. 

Mwisho... 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI