Header Ads Widget

MTANZANIA ALIYEKUWA ANAELEKEA CHINA AMSIFU DKT SAMIA AKIWA JUU YA ANGA NA NDEGE YA AIR TANZANIA.

Na Gift Mongi, Moshi

Watanzania wametakiwa kuendelea kuliamini na kutumia Shirika la Air Tanzania kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuliwezesha Shirika hilo.


Kauli hii inatolewa na mtanzania aliyekuwa akielekea nchini China Yuvenail Shirima  kwa ndege ya  shirika la Air Tanzania na kusifu jitihada za rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha shirika hilo.


Kwa mujibu wa video ambayo ina dakika 3 Shirima alitoa kauli hiyo akiwa njiani na kuwa watanzania kulipenda shirika hilo ni moja ya uzalendo na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuleta maendeleo 


Amesema serikali imekuwa ikiboresha miundombinu yake kila siku lengo likiwa ni kusogeza huduma zake kwa wananchi na kuwa kama watanzania tunatakiwa kuwa wazalendo kwa kuunga mkono kile kinachofanywa 


 'Sisi kama watanzania kwa sasa ni lazina tujivunie hivi vitu vizuri vinavyofanywa na rais Dkt Samia Suluhu Hassan na katika kumuunga mkono ni lazina tutumie ndege zetu ili kulifanya shirika kuendelea kuwa hai'amesema


Pia katika video hiyo, amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kujenga uhusiano mzuri wa kimataifa kati ya Tanzania na China ambapo wasafiri wanaingia China bila usumbufu wowote jambo linaloendelea kustawisha biashara kwa pande zote mbili

Aidha katika hatua nyingine  Shirima ambaye pia ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini 

amewataka watanzania kumuunga mkono rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha utalii nchini kwa kutumia shirika la ndege nchini.


'Tuunge mkono jitihada zinazofanywa na serikali kuhamasisha utalii lakini tuhamasishe pia kutumia kwa Shirika letu la ndege katika kukuza utalii'amesema


Ameeleza maendeleo mbalimbali yanayo fanyika nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vya mama na mtoto, madawa na vifaa tiba kuwa ni jitihada za serikali kuakikisha wananchi wanasogezewa huduma karibu yao.


Kadhalika  mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini  V amesema , Rais samia amewekeza kwa kwenye elimu nchini hali ambayo inawafanya watanzania kusoma bure kuanzia elimu ya msingi hadi secondari huku akitoa mikopo katika vyuo vikuu na kati.


Mdau wa usafirishaji katika sekta ya anga Michael Mwangano amesema kuendelea kutumia ndege za shirika letu la Air Tanzania ni uhamasishaji mzuri katika kukuza utalii hasa ule wa kimataifa.


'Kuna kipindi tulikuwa hatuna ndege inayoruka lakini sasa dunia inaanza kutuelewa vizuri hakika hapa kama taifa tumepiga hatua na serikali Ina haki ya kusifiwa katika hili'Amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI