Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI ASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU ALIYEPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA KUANGUKIWA NA MTI KUTOKANA NA MVUA KUBWA MKOANI KILIMANJARO.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 

Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Moshi zimeleta madhara baada ya kusababisha miti kungoka na kuleta umauti. 


Mnamo Novemba 27 mwaka huu katika kijiji cha Kirima kati kitongoji cha Ngirini Renatha Epimack Mushi ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijiji aliangukiwa na mti na kupelekwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC na kufariki Dunia Disemba 5 mwaka huu. 



Ajali hiyo ilitokea eneo la Ngirini katika Kata ya Kibosho Kirima,  jimbo la Moshi vijijini ambapo katika ajali hiyo, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kibosho Kirima Japhary Kway alinusurika kwa kuvunjika mkono na Bajaji yake kupondwa pondwa na mti huo.



Akiongea wakati wa kutoa salamu za rambirambi kwenye mazishi hayo, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi aliwapa pole wanafamilia na waombolezaji wote waliokuwa na huzuni na simanzi kutokana na tukio hilo la kutisha. 



Ndakidemi aliwaomba waombolezaji wote kumwombea marehemu ili roho yake ipumzishwe mahali pema peponi. 


Msemaji wa familia aliishukuru serikali kupitia kwa mkuu wa Wilaya, Kisare Makori kwa ushirikiano katika zoezi la kulipia sehemu ya matibabu ya marehemu hospitalini KCMC.



Mazishi hayo yaliongozwa na Padri Wilhelm Malasi  kutoka Parokia ya Mtakatifu Ana Kirima na yalihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini.



Prof Ndakidemi alijumuika na viongozi wa CCM Kata ya Kibosho Kirima na waombolezaji wengine katika kijiji cha Kirima Kati Kitongoji cha Ngirini. 


Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI