Header Ads Widget

KIMEI ATEKELEZA AHADI YAKE YA KUKARABATI CHOO NA KUREJESHA MAJI SOKO LA RINDIMA KATA YA KIRUA VUNJO MAGHARIBI

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


WAKATI wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 watumiaji wa soko la Rindima kata ya Kirua Vunjo Magharibi waliwasilisha kilio chao cha choo cha soko hilo kufungwa kwa sababu ya uchakavu na ukosefu wa maji kwa Dkt Charles Stephen Kimei akiwa katika kampeni za kuomba kura za ubunge wakati huo.


Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei alifika katika soko hilo akiwa ameambatana na Diwani wa kata hiyo, John Kessy, Diwani wa Viti Maalum Jenifer Nyambo, Mwenyekiti na Katibu wa CCM kata ya Kirua Vunjo Magharibi Baltazar Macha na Cain Chaky kwa ajili ya kuona utekelezaji wake ulipofikia. 



Wakiwa Sokoni hapo, Kessy amemshukuru Dkt Kimei kwa kuwezesha shilingi 7,390,000/- kwa ajili ya ukarabati, uwekaji wa tiles, kuweka mfumo wa maji, kulipia maji, kufunga mita, kuweka milango ya grili na kupiga rangi. 


Kazi zilizosalia ni ujenzi wa kuta za kuwapa faragha watumiaji wawapo eneo la choo pamoja na kuingiza maji sokoni ambazo zitakamilishwa wakati wowote kwa kuwa fedha ipo. 


"Kukamilika kwa choo hiki na kuanza kutoa huduma kutaimarisha usalama wa afya wa watumiaji wake".


Akiwa Sokoni hapo Dkt Kimei amewahakikishia wananchi kuwa ndani muda wa miaka mitatu zilizokuwa agenda za kata hiyo katika maendeleo zimetekelezwa ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya kituo chao cha afya cha Kirua Vunjo ambacho tayari kimepata majengo mapya baada ya kupewa shilingi milioni 50.



Ukamilishaji wa bwalo la chakula la Pakula ambalo yeye binafsi alichangia bati 78 na sasa wamepata shilingi milioni 30 kukamilisha Bwalo hilo toka Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na matengenezo ya barabara za Kiwaloni-Manu ambayo kazi imefanyika na Nduoni - Kilema ambayo kazi inaendelea. 


"Tutaendelea kutumika kwa uaminifu kukamilisha kile ambacho tuliahidi na kushughulika na kero mpya ili kuharakisha maendeleo yetu naomba muendelee kutuunga mkono." alisema Dkt Kimei



Naye diwani wa viti maalum, Nyambo amemshukuru Dkt Kimei kwa kazi nzuri ya maendeleo katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa maabara shule ya sekondari Iwa.


Wanawake sokoni hapo walipaza sauti za furaha wakisema wanashukuru sana kwa sababu walikuwa wanapata shida sana na choo hicho viongozi mbalimbali wa kisiasa wamekuwa wakiahidi kukifanyia ukarabati bila mafanikio.

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI