Na Pamela Mollel Arusha
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Mussa ameitaka kamati ya lishe kupanua wigo wa kutoa elimu kwa jamii ili kukabiliana na changamoto ya udumavu kwa watoto
Alitoa agiza hilo wakati akifungua kikao lishe Mkoa wa Arusha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Arusha
Mussa aliongeza kuwa licha kuwa changamoto ya udumavu kwa watoto inaendelea kupungua siku hadi siku bado kuna changamoto hiyo kwa watoto wa maeneo ya vijijini
"Uhaba wa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa lishe kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 2na miezi 7 hivyo ni vyema wataalamu pamoja na wadau kushirikiana kwa pamoja ili kuwafikia wananchi waliopo pembezoni"alisema Mussa
0 Comments