Na Shemsa Mussa,Kagera.
Aliyewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba lakini pia aliwahi kugombea nafasi ya Ubunge na pia ni Mwenyekiti Mpya wa wilaya Bukoba kupitia tiketi ya chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema Ndg Chief Kalumuna aeleza mikakati yake katika kuendelea kukuza chama hicho .
Akizungumza katika Mahojiano Maalumu Ndg kalumuna amesema anatoa shukurani zake kwa kamati pamoja na wanachama wote kwa kumuamini na kumpatia nafasi ya yeye kuwa Mwenyekiti ambapo amesema jumla ya wagombea walikuwa 3 na yeye aliweza kuibuka mshindi kwa kupata kura za ndio na kuweza kutangazwa kuchukuwa nafasi hiyo na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu John Mlema kwa kukiongoza chama kwa Miaka mingine Mbele.
"Chama chetu kilipitia mambo mbalimbali kwa miaka kama sita nyuma kwa maana hiyo aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya kwa Miaka 15 Ndg Victor Sherejei alipotangaza kun'gatuka katika nafasi hiyo wadau wa siasa na wanachama wa chadema waliniomba nichukue viatu vyake kwahiyo niliwiwa kugombea kwa ushawishi watu ,amesema Ndg Kalumuna "
Ameongeza kuwa walimuamini akichukua nafasi hiyo ataweza kuwaongoza vema na zaidi wakiwa wanaamini katika misimamo yake thabit katika chama hicho na kuamini atachukua na kukibeba chama kwa niaba ya wanachama pia na mapambano mbalimbali hasa ya uchaguzi wa serikali za Mitaa Mwaka 2024 na zaidi katika uchaguzi Mkuu wa 2025 pia kulinda maslahi ya Chama.
Aidha Ndg kalumuna amesema kwa sasa anao mtihani na kazi kubwa ya kurudisha imani ya kufanya chama kiweze kukubalika na kupata nafasi katika uchaguzi ujao pamoja na kurudisha historia za ushindi katika chaguzi mbalimbali kama miaka ya nyuma pia na kueema kuwa atayaendeleza yale mema yaliyofanywa na kiongozi aliyepita na yale yaliyo na mapungufu kidogo kwa kushitikiana na wenzake wataweza kufanya malekebisho ili kusonga mbele zaidi.







0 Comments