Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WAHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA

 

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR 

MWENYEKITI wa Chama cha ACT- Wazalendo Taifa Juma Duni Haji amewashajihisha Wazanzibar kuwa na muamko wa kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura ili kuwa na sifa halali ya kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

 

Wito huo ameutoa katika muendelezo wamikutano ya hadhara ya Chama cha ACT Wazalendo uliofanyika katika Jimbo la Pangawe Unguja ambapo amesema kwamba, Wananchi wanapaswa kujitokeza katika zoezi la uandishwaji ili kuwa na sifa za kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu.

 

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, amesema kwamba wazanzibari wanaendea kugubikwa na umasikini jambo linalopaswa lisiendelee kuwepo.

 

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Ismail Jussa amesema kwamba chama chake kitaedelea kueleza masuala  mbali mbali mbele ya umma ambayo wanaamini kwamba uendeshaji wake hauna manufaa kwa wananchi kama walivyofanya kwenye mikutano ya awamu iliyopita.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI