Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
Waziri wa Maji Juma Aweso ameitaka Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (DAWASA) kuwaunganishia maji wananchi ambao hawana uwezo wa kulipa moja kwa moja na badala yake wawakate kwenye bili zao, ambapo huduma hiyo wananchi wanatakiwa kuipata kwa wiki zisizo zidi mbili.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa kwenye hafla ya utiaji saini na makabidhiano ya eno la mradi wa ujenzi wa tanki la maji Bangulo ambapo mradi huo utaendeshwa na mkandarasi kutoka china M/S Sinohdro na kusimamiwa Mhandisi mshauri M/S Scet Tunisie kwa ufadhili wa benki ya dunia.
"Mradi huu wa usambazaji maji maeneo ya kusini mwa Dar es Salaam katika manispaa za Ubungo, Temeke, Kibamba pamoja na Jiji la Ilala mkoa wa Dar es Salaam ni muendelezo wa jitihada za kuboresha huduma ya maji katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji"amesema Waziri Aweso.
Amesema kuwa,Wizara ya maji haitokuwa kikwazo kwa mwananchi yoyote kutopata maji safi na salama, hivyo wananchi wanaotaka kuunganishiwa maji hata kama hawana fedha wakopeshwe watakatwa kwenye bili zao za maji.
Aidha, amesema hana mashaka na mkandarasi aliyepewa mradi, hivyo asimamiwe vizuri na atakapoomba fedha apatiwe kwa haraka kwani kila kitu kipo tayari, ambapo mradi huo anautarajia kukamilika kwa wakati kama makubaliano ya yalivyofanyika.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Dawasa Kiula Kingu amesema viongozi wao wanasimamia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) vizuri katika kutekeleza mradi wa maji Bangulo hivyo, watahakikisha wanautunza na kuvisimamia vifaa vizuri.
"Tarehe 20, mwezi wa 8, 2023 alikuja kutembelea Naibu Waziri wa Maji Merry Mahundi alitoa ahadi siku 90 mradi utaanza utekelezaji wake lakini leo tumeshuhudia utiaji saini wa mradi mkubwa wenye thamanibya bill 42 uliofadhiliwa na benki ya dunia "amesema Kingu.
Amesema kuwa, mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam unahusisha, Ulazaji bomba la chuma la kusafirisha maji kwa umbali wa kilo 10.8 kutoka kwenye kituo cha kusukuma maji kibamba mpaka kwenye lanki la Bangulo.
Ameongeza kuwa lengo la mradi huo ni kutatua changamoto za upatikanaji maji hasa kwa maeneo ya ilala, kibamba, Kisarawe,Ukonga, Segerea ubungo na Temeke, ambapo pia wameshakamilisha miradi midogo midogo ya maji.
Naye, Diwani wa Kata ya Pugu Station Shaban Mussa amesema hana shaka na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapimduzi (CCM) katika jimbo la ukonga kwani kwenye kila sekta wamepiga hatua ikiwemo Afya, Elimu, Miundombinu na kupitia mradinwa maji Bangulo wanakwenda kufanya vizuri zaidi kwa wananchi.
"Viongozi wetu wanasimamia ilani vizuri kupitia kupitia mradi huu tumeona, tutahakikisha tunautunza vizuri na kuvilinda vifaa kwa sababu tuna kiu kukamilika kwa mradi ili kuhakikisha wananchi wananufaika"amesema Shaaban.
0 Comments