WAHITIMU 191 wa chuo Cha Mafunzo ya ufundi Stadi na Huduma Iringa (VETA)wamemuomba mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada kusaidia Kufuatilia ahadi ya gari la chuo na ahadi nyingine zilizoahidiwa na mgeni rasmi Mahafali kama hiyo iliyofanyika mwaka jana.
Wahitimu hao wamefikisha ombi hilo leo wakati wa Mahafali ya 27 ya chuo hicho huku mgeni rasmi akiwa mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Walisema pamoja na changamoto mbali mbali zinazokikabili chuo hicho mwaka Jana wakati wa Mahafali aliyekuwa mgeni rasmi aliwaahidi kusaidia kutatua changamoto hizo ikiwemo ya gari la chuo .
"Kupitia changamoto tulizonazo ni pamoja na kutokuwa na basi la kusafiri ,vifaa vya michezo kama vile mipira ,jezi ,viwanja vya michezo hivyo tunaomba utusaidie kutatua Changamoto hizo ..mwaka uliopita mgeni rasmi alituahidi kutuletea gari ya Mafunzo ya udereva ya Mafunzo ya udereva,mipira 100,jezi za michezo jozi 3 pamoja na kutengeneza kiwanja Cha michezo ,Ndugu mgeni rasmi ombi letu kwako tunaomba utusaidie kwenda kumkumbusha atimize ahadi yake"
Wahitimu hao walisema kuwa chuo hicho kinakosa gari la Usafiri kwa ajili ya wanafunzi kwenda kwenye Mafunzo ya vitendo mbali mbali pamoja na michezo hivyo kukosa hamasa ya kujituma katika michezo na kujifunzo kupitia Mazingira tofauti .
Kwa upande wake Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akijibu maombi hayo ya wahitimu alisema atahakikisha anamfuatilia Mdau huyo Ili kutimiza ahadi zake kama alivyo ahidi .
Aidha alisema kwa upande wa changamoto nyingine hasa zile za uhaba wa vifaa vya Mafunzo alisema vifaa hivyo Serikali itaendelea kutekeleza na pia kuwataka wanafunzi wanaopata Fursa za masomo kusoma kwa Juhudi zaidi .
Alisema kuwa elimu inayotolewa VETA ni elimu Nafuu zaidi ukilinganisha na maeneo mengine hivyo anaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuendelea kuchangia gharama ya Mafunzo katika Vyuo vya VETA .
0 Comments