Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
BAADHI ya wafanyabiashara katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameitaka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkoa wa Kilimanjaro kuongeza utoaji wa elimu juu ya mlipa kodi na ufanyaji wa biashara ili kuwepo muamko wa wafanyabiashara kulipa kodi na sio kutumia vitisho kama wanavyofanya baadhi ya watumishi wao.
Akizungumza jana mara baada ya uzinduzi ya wiki ya Shukurani kwa mlipa kodi Yashiva Shan, alisema asilimia 80 ya walipa kodi bado hawana utayari wa kulipa kodi na badala yake hulipa kutokana na kuogopa vitisho.
Shan alisema wataalamu hao, wanapofika katika biashara, hawana lugha za kuelimisha na badala yake kutoa vitisho na wakati mwengine kuwataka kulipa fidia jambo ambalo linajenga hofu.
"Leo wamesema wamefikia malengo na kuvuka, hatuwezi kuwapa hongera kwani kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Kilimanjaro wangeweza kukusanya zaidi endapo wangekuwa lugha za ulimishaji,
Wakati mwingine hudai wafanyabiashara wanageuka mimi nashauri kutokana na uhali ya utafutaji, waunde magroup ya wafanyabiashara kutokana na biashara zao, Mfano vipodozi, vileo ambapo kila mara kwa kushirikiana na wataalamu wengine wanaonyesha fursa za masoko, namna bora ya kukaribisha wateja na kisha namna ya kufunga hesabu hii ingesaidia ulipaji wa kodi kwa hiyari tofauti na ilivyo kwa sasa wanachukua wasipojua vilipotoka,"alisema Laura Mushi
Hosiana Msuya mfanyabiashara wa vipuli vya magari alisema licha ya wataalamu hao kutoa elimu ila bado haikidhi hitaji la wafanyabiashara.
"Yawezekana ikawa nje ya uwezo wao, ila ni wakati umefika serikali kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wafanyabiasha kuhusu uzalishaji, usambazaji, uuzaji wa bidhaa ili kuleta faida itakayomuwezesha mtu kulipa kodi kwa hiyari,sio kutoa elimu ya kodi tu haimsaidii mfanyabiashara "alisema Hosiana.
Aidha akisoma risala yake kwa mgeni rasmi Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro James Jilala alisema Mamlaka hiyo imekusanya zaidi ya bil.263 kwa mwaka 2022/23 ambayo ni zaidi ya asilimia 100 kutoka kwenye lengo lilokusudiwa bil.257 kwa kipindi kilichopita.
Alisema katika mwaka wa fedha unaoendelea, tayari wamekusanya bil.71 sawa na asilimia 72 ya lengo la kukusanya bil.76 kwa kipindi cha julai hadi Oktoba 2023.
"Jitihada hizi ni ushirikiano wa pamoja kati ya watumishi pamoja na walipa kodi, ila tunakabiliwa tatizo la magendo katika maeneo mbalimbali, yakiwemo Chekereni na Kahe hali inayopelekea upotevu wa mapato.Tunamikakati kwa kushirikiana na taasisi za kiserikali za kuhakikisha tatizo hilo linakomeshwa,"alisema Meneja.
Nae mgeni rasmi katika wiki hiyo, mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori alisema ajenda yankuongeza mapato ni la lazima na kuzitaka mamlaka husika kuongeza hali ya upatikanaji wa magari ya Doria ili kudhibiti hali hiyo.
"Wafanyabiashara tulipeni kodi hii ndio msingi wa maendeleo ya taifa letu, na ikiwa kunamatatizo katika mfuno tuleteeni na tutayafanyia kazi kwa kuwasilisha katika ngazi husika na tatizo hilo litageuka historia," alisema Mkuu wa wilaya.
Mwisho.






0 Comments