Header Ads Widget

TV 15 ZAIBWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA NJOMBE



Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka mwenye shati akiwa kwenye kontena lililoibiwa TV 15 Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe



Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima APP NJOMBE


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Njombe Antony Mtaka ambaye ni mkuu wa mkoa ameagiza kusimamishwa kazi watumishi wa Idara za Manunuzi,Tehama na Katibu wa Afya katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe kutokana na tuhuma za wizi wa Tv 15 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11 na kompyuta 3.


Mtaka ametoa agizo hilo akiwa katika Hospitali hiyo kufuatiwa kuwapo kwa taarifa za wizi wa vifaa hivyo tangu mwezi wa saba mwaka huu bila kuripotiwa kwenye chombo chochote cha ulinzi na usalama huku idara ya Tehama ikishindwa kutambua chochote kutokana na Camera kutofanyakazi.


Wizi huo umeripotiwa kufanyika kwa kufungua kontena lililokuwa na vifaa hivyo katika siku ambazo sio za kazi na baada ya kubainika tatizo hilo mkuu wa Idara ya manunuzi wa Hospitali hiyo pamoja na watunza funguo wenzake wakamua kukubaliana kuzilipa kwa kwenda kumuomba  mfanyabiashara wa vifaa vya umeme  mjini Njombe ili awape Tv 15 nyingine ambazo watazilipa katika siku za usoni.

Baadhi ya watumishi Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe wakichukuliwa maelezo na vyombo vya usalama


Awali mganga mfawidhi wa Hospitali Hiyo Dokta Winfred Kyambile amesema hatua alizochukua baada ya wizi huo ni kuwaita wote na kuwahoji lakini hakuripoti polisi.


Watuhumiwa wa wizi wa vifaa hivyo akiwemo mkuu wa Idara ya Manunuzi Aloyce Kavumika wamesema siku ya tukio wote hawakuwepo kwani walikuwa nje ya mkoa na hivyo walipigiwa simu kuwa kontena lipo wazi na TV Zimeibiwa.


Kwa upande wake Katibu tawala Rasilimali watu mkoa wa Njombe Lewis Mnyambwa amekiri kupokea maagizo ya mkuu wa Mkoa na kuahidi kwenda kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi hao kwa mujibu wa sheria.


Hata hivyo imeelekezwa kufungwa kwa mifumo ya Camera katika Hospitali hiyo kupitia maofisa tehema wengine ili kuongeza ulinzi katika Hospitali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI