NA HADIJA OMARY, LINDI
Watu 14 wamepoteza maisha na wengine 26 kujeruhiwa kufuatia ajali ya Basi la kampuni ya Baraka lenye namba ya usajili T336 DPW lililokuwa linatokea Wilayani Newala Mkoani Mtwara kuelekea jijini Dar es salaam kufeli breki na kuanguka katika eneo la Mputa maarufu kama kona ya Nyale,katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi
Akizungumza leo Jumapili Novemba 26.2023,kamanda wa polisi Mkoa walindi ACP John Makuri amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa1:10 Asubuhi ya leo ambapo dereva wa Kampuni ya BARAKA CLASSIC lenye namba za usajiliT336DPW, gari lilikuwa linatokea Newala kwenda Dar es Salaam
Kamanda amefafanua kuwa vifo 12,vilikuwa vya abiria waliokuwa ndani ya basi hilo huku vifo vya watu wawili walikuwa Watembea kwa miguu,na majeruhi 26,wanapatiwa matibabu katika hospitali ya nyangao
"Watu hao 14 waliofariki,12 ni abiria waliokuwa wanasafiri na basi hilo ,na wawili walikuwa Watembea kwa miguu,dereva wa basi la baraka anapatiwa matibabu,katika hosptali ya Nyangao akiwa chini ya ulinzi".Amesema kamanda Makuri
Pia kamanda Makuri ametoa wito kwa madereva ambao wazembe,nakusema kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya madereva wazembe ambapo amesema kuwa ,madereva wanadhamana kubwa ya maisha ya abiria ambapo pia amesema dereva alikuwa anajua kama gari lina hitilafu lakini bado alikubali kuendesha.
Moja ya mashuhuda wa ajali hiyo Juma Machalila amesema wakati wa zoezi la uokoaji walitokea nyuki na kulifanya zoezi la uokoaji kuwa gumu kutokana na nyuki hao.
"Nyuki hao wapo siku zote ila baada ya kutokea ajali walianza kung'ata watu nakuanza kukimbia tukalazimika kununua dawa ya wadudu (dawa ya rungu) pamoja na kuchoma matairi ,vifo vilivyotoÄ·ea ni sababu moja wapo ya watu kukosa msaada kwa haraka"amesema Machalila.
Naye diwani wa kata ya Mtama halmashauri ya Mtama Maria Nyale amesema kuwa gari hilo lilikuwa limefeli breki na kwenda kusababisha watu zaidi ya 14 kufariki.
"Tukio kubwa lililo tokea baada ya ajali kutimka kwa nyuki,walitimka sana ikasababisha kushindwa kuwaokoa watu lakini polisi walifika mapema wakashirikiana na wananchi kuchoma mipira nyuki wakatoka na zoezi la uokoaji likaendelea ,ambapo watu 14 wamefariki "amesema Nyale.
Nae Mkuu waMkoa wa lindi Zainabu Telack,amewashukuru wananchi waliosaidia kuokoa pindi ajali ilipotokea ambapo baada ya kutokea ajali nyuki wengi walitokea na kusababisha baadhi ya wananchi kuumwa na nyuki na kupelekwa hosptali.
"Niwashukuru sana wananchi wa Mtama kwa juhudi mliofanya ya uokoaji pindi ajali ilipotokea licha ya kwamba kulikuwa na nyuki wengi"Amesema Telack
0 Comments