Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP.
SERIKALI imefanya mjadala wa namna bora ya kutekeleza Sera ya urejeshaji wa Shule wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda alipokutana na kufanya mazungumzo na timu ya ujumbe wa UNICEF ukiongozwa na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Bi Eike Wisch Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo ya Viongozi hao wamejadili kuhusu Sera ya urudishwaji wa wanafunzi waliokatizwa masomo kutokana na sababu mbalimbali kama vile utoro, utovu wa nidhamu, kupata ujauzito na walioshindwa kuhudhuria masomo kwa muda mrefu.
Walisema katika mjadala huo kuwa uamuzi huo wa kuwarejesha shuleni wanafunzi hao umewapa fursa kupata elimu ambayo ni haki ya msingi na kuwasaidia kukamilisha mzunguko wa elimu katika mfumo rasmi wa elimu.
Aidha, viongozi hao wamejadili namna bora ya utekelezaji wa Sera hiyo ikiwa ni pamoja na kuwezesha tafiti mbalimbali za kubaini na kuendeleza afua zenye kujielekeza katika kupunguza tatizo la mdondoko wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na ujauzito kwa wanafunzi wa kike.
0 Comments