Header Ads Widget

PROFESA NDAKIDEMI AZITAKA TARURA NA TANROAD KUSIMAMIA FEDHA ZINAZOLETWA NA SERIKALI THAMANI IONEKANE..

 



NA  WILLIUM PAUL, MOSHI. 

MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi amesema kuwa siasa za Moshi na mkoa wa Kilimanjaro ni barabara na kuwaomba wakala wa barabara mijini na Vijijini (Tarura) pamoja na Tanroad kuhakikisha wanasimamia fedha zinazotolewa na serikali ili thamani ya fedha zionekane. 


Prof. Ndakidemi ametoa kauli hiyo katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Kilimanjaro ambapo alitumia nafasi hiyo kuzipongeza Tarura na Tanroad kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha barabara zinapitika muda wote.



Alisema kuwa, ipo haja kwa taasisi hizo zinapojenga barabara zihakikishe zinajenga na mifereji ya maji mvua ili kuhakikisha barabara hizo zinadumu muda mrefu. 


"Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya miundombinu ya barabara hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha tunasimamia fedha hizo ili zioneshe matokeo pia hakikisheni mnajenga mifereji ya maji ya mvua ili kulinda barabara zetu" Alisema Prof. Ndakidemi. 



Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuomba kuharakishwa kwa ujenzi wa barabara ya Getifonga-Mabogini ambapo ipo kwenye Ilani ya uchaguzi. 


Aidha Mbunge huyo alitumia kikao hicho kuwaomba Tanroad na Tarura kuona haja ya kufanya mgawanyo sawa wa barabara za lami huku pia akitumia nafasi hiyo kuziombea barabara za kuelekea katika mlima Kilimanjaro ambapo zimekuwa zikitumiwa na watalii zianze kufikiriwa na kuwekewa lami ili kurahisisha watalii kupita.


Katika hatua nyingine amewaomba Tarura kuona haja ya kukamilisha barabara ya Rafaeli-Kncu kwa kiwango cha lami. 

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI