Header Ads Widget

NIRC YAOMBA SERIKALI ISAIDIE KUDHIBITI UVAMIZI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI MSINGI

Na Thobias Mwanakatwe, SINGIDA

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imesema mradi wa skimu ya umwagiliaji uliopo kijiji cha Msingi kata ya Msingi wilayani Mkalama mkoani Singida ambao serikali imetoa zaidi ya Sh. bilioni 34 kuutekeleza huenda ukapoteza maana kufuatia wananchi kuanza kuvamia eneo la kilimo kwa kujenga nyumba za kudumu za kuishi.

Mkurugenzi wa NIRC, Raymond Mndolwa, aliwaeleza jana wabunge wa Kamati ya Bunge ya Bajeti walipotembelea mradi huo kwa ajili ya kujionea maendeleo ya ujenzi ambao utakapokamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya wakazi 12,000 wa vijiji vinne vilivyopo kata ya Msingi.

"Wananchi wameanza kujenga nyumba na sasa tumeanza kupoteza eneo la kilimo,uwekezaji uliofanyika thamani yake eneo la kilimo lazima libakie lile lile vinginevyo manufaa ya uwekezaji huu haitapatikana," alisema.

Mndolwa aliwaomba viongozi wa serikali ya wilaya na mkoa iingilie kati suala hili kwa kuwazuia wananchi wasiendelee kujenga mashambani kwani Sh bilioni 34 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mradi huu ni fedha nyingi.


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Silo, alisema miradi ya umwagiliaji inayotekelezwa ni kwa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anataka kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa wananchi na pato la taifa kwa ujumla. Silo aliwataka wananchi wasijenge kwenye eneo la mradi hasa kwenye mashamba yanayotarajia kulimwa kwani mradi huu ukikamilika utawanufaisha wao kwa kulima zaidi ya mara moja kila mwaka.

Aidha,aliiomba Wizara ya Kilimo hasa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji isimamie mradi ukamilike kwa wakati kwani nia ya rais ni kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo hivyo kila mwenye jukumu ka kusimamia afanye hivyo ili ikamilike kwa wakati na hivyo kuleta tija.

Aidha,aliiomba Wizara ya Kilimo hasa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji isimamie mradi ukamilike kwa wakati kwani nia ya rais ni kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo hivyo kila mwenye jukumu ka kusimamia afanye hivyo ili ikamilike kwa wakati na hivyo kuleta tija.


Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, alisema serikaki inataka wananchi walime si kwa kutegemea mvua na kwamba mradi huo utakapokamilika utaongeza pato la mwananchi sababu atakuwa anavuna zaidi ya mara mbili kwa mwaka na pia itaongeza pato kwa halmashauri na usalama wa chakula nchini. Silinde akizungumzia suala la wananchi kuanza kujenga katika mashamba ni kwasababu wanafahamu nini kinakwenda kutokea na kuwataka waache serikali itengeneze miundombinu ya mradi huu kwani lengo la serikali ni kuondokana kwenye kilimo cha kienyeji kuja kwenye kilimo cha kisasa chenye tija.

Awali Mkurugenzi wa Idara ya Ukarabatu na Ujenzi sa Miundombinu, Mhandisi Fuko Koyoya, alisems mradi huu ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 utawanufaisha wakazi 12,000 wa vijiji vinne vya Ishinsi, Ndurumo, Msingi na Kidi vilivyopo Kata ya Msingi tarafa ya Kinyangiri ambao watalima mazao ya mpunga,mahindi na mbogamboga Kwa misimu miwili hadi mitatu kwa mwaka, Alisema shughuli zitakazofanyika katika mradi huu ni ujenzi wa bwawa lenye ujazo wa Lita 1,875,000, ujenzi a mifereji ya umwagiliaji yenye kilometa 19.12, uchimbaji wa mifereji ya matupio yenye urefu wa kilo mita 42.539, uchimbaji wa mifereji ya kuingiza Maji mashamba yenye urefu wa jumla ya kilometa 34.778.



Shughuli nyingine zitakazofanyika ni ujenzi wa barabara za mashamba zenye urefu wa kilomita 36.1, kusawazisha ekari 2.000 za mashamba, ujenzi wa kilomita nane za barabara na makaravati sita kuelekea ndani ya mradi na ujenzi wa vigawa Maji 14.vipunguza mwendo, viumbo angalizi 90,vipitisha maji 90, makaravati 14 pamoja na vivuko nane. Mradi huo ambao umeanza kujengwa Julai Mosi mwaka huu unatarajia kukamilika Disemba 14, 2024.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI