Header Ads Widget

NGAJILO AWATAKA MAKADA CCM KUGOMBEA NAFASI SERIKALI ZA MITAA

NA RAYMOND MINJA MATUKIO DAIMA APP,MAFINGA 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi(CCM) mkoa wa Iringa Fadhili Ngajilo amewataka makada wa CCM   kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba ,2024.


Akizungumza na wananchi ,makada wa chama hicho  kwenye kata ya Boma  wakati wa ziara ya kamati ya  utekelezaji wazazi mkoa wa Iringa ziara yenye lengo  kuhuisha jumiya kwa kuongeza wanachama Ngajiro alisema kuwa ni muhimu makada wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hizo .



 Ngajilo alisema  kuwa jumuiya ya Wazazi ni jumuiya kubwa nchini hivyo ni lazima watu watambue umuhimu wa jumuiya hiyo sambamba na kuchukua kadi kwa wingi ili kujiunga katika jumuiya hiyo.


Hata hivyo Ngajilo aliwata  Wananchi na Wanachama kujiunga na jumuiya hiyo sambamba na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi ujao kuanzia ngazi za serikali za mitaa na nyinginezo huku wakitekeleza kauli ya chama ya Tripple T ya Chama yaani “Tutashiriki, tuwashirikisha, tutashirikiana” 


Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ua Utekelezaji Mkoa wa Iringa ambaye pia ni mlezi wa  Wazazi Wilaya ya Mufindi , Charles Makoga alisema kuwa mpango mkuu wa Chama ni kushinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao kuanzia serikali za mitaa na ngazi nyinginezo hivyo Wananchi wanapaswa kutokuwa na matabaka kwani yatapelekea kutengana na kukigawa chama.


Kaimu Katibu wa Jum


uiya ya Wazazi Mkoa Wa Iringa, Anitha Magelanga aliwataka Wananchi kujipanga zaidi kwa uchaguzi ujao pamoja na kupiga vita aina zote za ukatili ambazo zinatokea katika jamii kwani wao kama Jumuiya ya Wazazi wanalaani aina zozote za ukatili huku wakishirikiana na taasisi nyinginezo kama vile Dawati la jinsia, Polisi na mengineyo.


 Ziara ya kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Iringa iliyofanyika katika Kata ya Boma tawi la Ihongole ilidhamiria kutoa shukrani kwa Wananchi, kuzungumzia uhai wa Jumuiya ya Wazazi, utekelezaji wa Ilani ya Chama sambamba na kuhamasisha wanachama wa CCM kujitokeza katika uchaguzi ujao, kupiga vita Ukatili katika jamii pamoja na ugawaji wa Kadi za jumuiya kwa Wanachama ambapo Kadi zilizotolewa mkoa mzima ni elfu mbili huku kadi 107 katika kila kata.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI