Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI OFISI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI NA UTAWALA BORA AISHUKURU DAWASA KWA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI CHALINZE

Na Matukio Daima Chalinze

MBUNGE wa Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete ameishukuru serikali na  Uongozi wa Wizara na DAWASA kwa kutatua tatizo la Maji katika halmashauri ya Chalinze. 


Hayo ameyasema mbele ya Kamati ya Bunge ya Mitaji kwa Umma, Mbunge huyo wa Chalinze amewashukuru pia kamati kwa niaba ya Bunge kwa jinsi walivyosimamia kuhakikisha tatizo Unaondoka kwa kupitisha bajeti ya Wizara ya Maji.


Naye Mtendaji Mkuu wa DAWASA , Injinia Kingu, Mbunge wa Chalinze alimshukuru kwa kutenga pesa kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara jimboni hapo mwaka jana. 


Katika ziara hiyo Rais Samia alielekeza  kutengwa kwa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya mradi wa Kusambaza maji katika mji wa chalinze na viunga vyake. DAWASA wametenga Shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya usambazaji Halmashauri ya Chalinze ikiwa ni mara mbili ya maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI