Header Ads Widget

MNEC MWAKITINYA AWATAKA BODABODA KUWA LINDA WATOTO WA KIKE.

 



NA WILLIUM PAUL, SAME. 


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Mussa Mwakitinya amewataka madereva usafirishaji (bodaboda) kuhakikisha wanawalinda watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao 



Mnec Mwakitinya ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na madereva bodaboda wa Tarafa ya Mamba vunta jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kuwa serikali inatambua kazi na juhudi kubwa zinazofanywa na Vijana hao. 


"Wapo Vijana kupitia bodaboda wamefanya mambo makubwa ikiwemo kujenga makazi, kusomesha watoto na wanaendesha maisha yao hivyo serikali inatambua mchango wenu katika kuleta maendeleo" amesema Mnec Mwakitinya. 


Na kuongeza "niwaombe kupitia kazi yenu hii walindeni sana watoto wa kike waweze kufikia ndoto zao hivyo kuweni mstari wa mbele kupambana na wale wote wenyenia hovu ya kuwakatika ndoto zao"


Aidha Naibu Katibu huyo alisema kuwa, kazi kubwa ya chama cha Mapinduzi kupitia UVCCM ni kuwasemea Vijana na kuahidi kuhakikisha wataendelea kuwasemea ili kuhakikisha Vijana wanapata maendeleo. 


Katika hatua nyingine Mnec Mwakitinya alitumia nafasi hiyo kuwataka Vijana na wananchi wa jimbo la Same mashariki kuendelea kuweka imani kwa Mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecella kwani amekuwa akipambana kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele katika jimbo hilo. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI