Header Ads Widget

MKUU WA MKOA WA MTWARA AZINDUA MAFUNZO YA MADEREVA NA MAAFISA USAFIRISHAJI.

Matukiodaima APP, Mtwara

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas  amezindua mafunzo ya siku tano ya madereva na maafisa usafirishaji kutoka mikoa mbalimbali nchini yanayoratibiwa na Chuo Cha Taifa cha usafirishaji  NIT ambapo amepongeza chuo hicho kwakutoa mafunzo hayo ambayo yatasaidia watumishi hao kwenda na wakati. 


Akizungumza wakati mafunzo hayo yakiendelea amesema kuwa mfumo wa utaoji wa mafunzo wa chuo hicho utaleta mabadiliko makubwa nchini katika sekta hiyo kutokana na ujio wa magari mapya ya teknolojia kubwa huku nchi ikiwa na uboreshaji mkubwa wa miundombinu. 

"Mafunzo haya yatatoa elimu ya kisasa kwakuzingatia wakati tulionao amapo naamini madereva hao wanaweza kutunza vizuri magari na vifaa iliviweze kudumu kulingana na mabadiliko ya teknolojua kulingana na magari yenyewe barabara tusipokuwa makini na mabdiliko haya tutakuwa chanzo cha kusababisha ajali" alisema Kanal Ahmed 


Naye Makamu Mkuu wa chuo cha NIT aneyeshughulika na masuala ya taaluma Dkt. John Mahona alisema kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo katika nyanja mbalimbali wakiwakumbusha maafisausafirishaji na madereva wajibu wao na namna sahihi ya kuisaidia serikali kupunguza gharama kwenye magari. 


"Serikali ina magari mengi sana na hivyo ni muhimu kwa madereva na maafisa usafirishaji kupata mafunzo ya kutumia magari vizuri, kutumia vipuli vizuri na kutumia vialainishi vizuri ili serikali iweze kupunguza matumizi  ambayo ni makubwa sana katika magari na yaachukua ghama kubwa pia" alisema Dkt. Mahona

Nae Afisa usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Samson Lugusi  alisema kuwa mafunzo ni mazuri kwetu na yanatukumbusha wajibu wetu hususani usimamizi bora wa sekta hii muhimu kwa Taifa.  


"Unajua dereva unaweza kumuelekeza  lakini akiwa barabarani anakuwa mwenyewe inakuwa ni changamoto ambapo husababisha ajali kutokana na mwendo kasi ambapo wakati mwingine husababisha ulemavu ambao sio wa lazima sisi kama maafisa usafirishaji tunaweza kupambana kupunguza gharama za uendeshaji tu" alisema Lugusi 

kwa upande wake dereva wa shirika la umeme Tanzania TANESCO Stanley Mligo ameeleza namna mafunzo hayo talivyo muhimu kwao na pia jinsi yatakavyowasaidia kutunza magari wanayoyaendesha. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI